PROF. MBARAWA: NEEMA YAJA WAFANYABIASHARA KANDA YA ZIWA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:06 AM
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akielekea kukagua Bandari ya Kemondo mkoani Kagera ili kujionea utendaji
kazi wake. Kulia ni Meneja wa Bandari Kanda ya Ziwa, Bw. Abel Moyo.
Meneja
wa Bandari Kanda ya Ziwa, Bw. Abel Moyo, akimuonesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), njia
ya reli katika bandari ya Kemondo mkoani Kagera, ambayo itaruhusu mizigo
itakayokuja kwenye mabehewa kwa njia ya meli iweze kupakuliwa na
kupelekwa kuhifadhiwa kwenye maghala.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua
sehemu ya maegesho ya meli katika Bandari ya Kemondo, mkoani Kagera.
Bandari hiyo ina upana wa mita 100.
Muonekano wa gati ya meli katika Bandari ya Kemondo, mkoani Kagera.
Kaimu
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani Kagera Eng.
Zephrine Bahyona, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa nne kulia), alipokuwa akikagua
Kivuko cha Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabasa, mkoani
Kagera.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani
Kagera Eng. Zephrine Bahyona, alipotembelea na kukagua kivuko cha
Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabasa, mkoani Kagera.
Muonekeano
wa kivuko cha Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabasa,
mkoani Kagera. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba watu sitini au magari
mawili madogo kwa wakati mmoja.
………………..
Imeelezwa
kuwa kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Umoja kutarudisha huduma ya
usafirishaji wa mizigo katika kanda ya ziwa kupitia bandari ya Kemondo
iliyopo mkoani Kagera.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa, wakati akikagua Bandari hiyo kuangalia maendeleo yake,
na kuitaka Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli Nchini
(TRL), na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), kuanza kuandaa Mfumo mmoja
wa kutoa Stakabadhi ili kuwarahisishia wateja wake huduma za
usafirishaji wa mizigo.
Aidha,
Waziri Mbarawa ameitaka TRL kukarabati njia za reli bandarini hapo
haraka iwezekanavyo ili kuruhusu mizigo itakayokuja ikiwa kwenye
mabehewa kwa njia ya meli iweze kupakuliwa pindi Meli hiyo itaposhusha.
“Serikali
imefanya ukarabati wa meli ya MV Umoja ambayo itabeba mizigo ikiwa
kwenye mabehewa na reli hii inahitaji ukarabati mapema ipasavyo
nawaagiza TRL kufanya ukarabati wa reli ili kusiwepo usumbufu wowote
wakati wa kushusha na kupakia mizigo hiyo” , amesema Profesa Mbarawa.
Ameiagiza
Mamlaka hiyo kuanza kutafuta tena wateja ambao kwa muda mrefu walikuwa
wamepotea kutokana na bandari hiyo kusuasua kutoa huduma zake kwa muda
mrefu.
Kwa
upande wake Meneja wa TPA Kanda ya Ziwa Bw. Abel Moyo, amemuahidi Waziri
huyo kutekeleza agizo lake kwa kushirikiana na TRL pamoja na MSCL na
kuwahakikishia wafanyabiashara wa kanda ya ziwa kuwa na matumaini mpya
ya kupata usafiri bora na wa uhakika.
Katika
hatua nyengine, Waziri Mbarawa ametembelea na kukagua Kivuko cha
Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabasa na kumtaka Kaimu
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoani humo, Eng. Zephrine
Bahyona, kutoa huduma bora sambamba na kukusanya mapato ili kuweza
kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili.
Naye,
Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoani humo Eng.
Zephrine Bahyona, amezitaja baadhi ya changamoto zinazoathiri utendaji
mzuri wa kivuko hicho kuwa ni kukatika kwa magugu maji na hivyo
kupelekea kusombwa kwa kivuko.
Waziri
Profesa Mbarawa pia amekagua barabara ya Uyovu- Bwanga yenye urefu wa
kilometa 45 mkoani Geita na kuridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa ujenzi
wa barabara hiyo ambapo ujenzi wake kwa sasa umefika asilimia 56.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WIzara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: