MADAKTARI BINGWA WA MOYO KUTOKA HOSPITALI YA SAIFEE YA INDIA NA WENZAO WA JKCI WAFANYA UPASUAJI KWA WAGINJWA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:50 AM
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Saifee ya
nchini India wakimfanyia upasuaji mgonjwa anayesumbuliwa na tatizo la moyo leo Machi 27, 2017. Baada ziara
aliyoifanya nchini mwishoni mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madheebu ya
Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao
watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa wagonjwa. Timu ya
wataalam hao ambao idadi yao ni sita imeshawasili nchini na tayari
wameanza kufanya upasuaji ambao utachukuwa siku tano na wanatarajia
kufanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza
katika mishipa ya moyo iliyoziba ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) na
upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo inamatatizo na inahitaji
kubadilishwa kwa wagonjwa 15. (PICHA NA ANNA NKINDA-JKCI)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: