NGEZE AKIRI MBELE YA RC MKOA WA KIGOMA HAWEZI KUACHA KULIMA BHANGE

Inline images 1

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Marco Gaguti akijiandaa kufyeka shamba la bhange la  mzee Yothamu Ngeze katika Pori la akiba la Maker kusini wilayani kasulu ( Picha na Magreth Magosso, Kigoma)
 

Na Magreth Magosso,Kigoma

Mkulima Mmoja mkazi wa wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma Yotham Ngeze amekiri kutoacha kulima zao hilo, kutokana na faida anayoipata kupitia  bhange na anapovuta hulima zaidi ya hekari moja ya shamba la chakula kwa kuwa alianza kufanya hivyo tangu mwaka 1973.


Akizungumza jana( juzi ) na wandishi wa habari  baada ya kushikwa na kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo katika operesheni ya kuteketeza  hekari moja ya mimea ya bhange ,Ngeze alisema alianza kilimo hicho tangu Mwaka 1973 wakati akiwa kibarua katika mashamba ya mkonge enzi hizo mkoani Tabora.

Alisema zaidi ya miaka 40 amekuwa ni mkulima wa mmea huo,ambao analima na kuutumia binafsi kwa ajili ya kuongeza nguvu mwilini ,ambapo anauwezo wa kulima shamba zaidi ya hekari moja kwa siku sanjari na kumpatia kipato cha ziada.

Kwa upande wa vijana waliokuwa wakisaidia kulima shamba hilo akiwemo ,Simoni Ndiyaimana alisema wamekuwa wathirika wa mmea huo tangu washiriki katika ulimaji wa zao hilo,ambapo bila kutumia mmea huo hawawezi kuishi kwa amani na kukiri inaathiri afya kwa kuwa wanafanya kazi kupita uwezo wao.

Akifafanua hilo,Kaimu Mkuu wa wilayani kasulu Kanali Marco Gaguti alisema serikali haina huruma kwa wakulima wa bhange na watumiaji wa mmea huo,na watuhumiwa wanne waliohusika katika ulimaji wa shamba hilo watachukuliwa hatua za kisheria  na kuwaaasa wananchi waepuke matumizi yam mea huo ambao unaathiri afya za walengwa.
“ mbaya zaidi mnatumia vijana kutoka nchi ya burundi ambapo wengi hushindwa kuwalipa fedha ,hatimaye kunatokea uhalifu kwa kisa cha kulipa kisasi ,matumizi ya bhange ni chachu ya ujambazi wa kutumia silaha na uporaji wa mali za umma,acheni kilimo haramu” alilalamika Kanali Gaguti.
Akitoa takwimu za mafanikio ya operesheni ya kuteketeza kilimo hicho Kamanda wa Polisi mkoani kigoma Ferdinand Mtui alieleza kuwa kwa kipindi cha mwezi Machi,mwaka huu hekari Saba za bhange na watuhumiwa Nane wanashikiliwa na vyombo vya usalama.
Alisema walifanikiwa kuchoma moto  hekari sita za shamba la bhange katika Wilaya ya Kakonko na Hekari moja katika Wilaya ya Kasulu huku wakiendelea na  msako wa wananchi wanaojihusisha na ulimaji wa zao hilo,ili kutokomeza biashara na matumizi yam mmea huo.
 

0 comments: