TANZIA

 Dkt. Dickson Nahimana Sahini (1982-2024)


Rais wa Chama cha Waatalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Gemma Berege anasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wa TDA, Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Daraja la kwanza (1) na Mkuu wa Idara ya Kinywa na Meno katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula (Ligula RRH) Mtwara, kilichotokea Januari 5, 2024 

Ratiba ya mazishi
Leo Jumapili (07 Januari 2024), Saa Nane (8) mchana mwili wa Marehemu Dkt. Sahini uliagwa katika Hospitali ya Ligula RRH alipokuwa akifanya kazi. 

Mwili wa Dkt. Sahini ulikabidhiwa kwa familia Saa Tisa (9)  mchana ikifuatiwa na misa ilifanyika nyumbani kwa Marehemu eneo la Mangamba, Mtwara. 

Saa kumi na mbili (12) jioni mwili ulianzasafari kuelekea Mkoani Ngara kupitia Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa. 

Siku ya Jumatatu (Januari 08 2024 baada ya kuagwa Dar es Salaam (Mbagala Chamazi majira ya Saa mbili asubuhi na kuondoka saa tatu), mwili wa marehemu Dkt. Dickson utaelekea nyumbani Ngara kwa ajili ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

TDA INATOA POLE ZA DHATI KWA FAMILIA YA MAREHEMU DKT. DICKSON SAHINI, WANATASNIA WOTE WA KINYWA NA MENO TANZANIA, NDUGU,  JAMAA NA MARAFIKI WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe.

0 comments: