NA KHAMISI MUSSA, DAR ES SALAAM.
Zaidi ya wanazfunzi 300 kutoka nchini
Marekani kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi kwenye huduma za afya na
wataalamu wa Hospitali ya JK iliyopo Kigamboni Dar es Salaam ikiwa ni mara ya
15 tangu waanze kubadilishana ujuzi huo.
Mafunzo hayo yameanza leo Juni 13,
2025 katika Hospitali ya JK ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt.
Telesphory Kyaruzi amewashukuru Wamarekani kwakuja kubadilishana ujuzi na
wataalamu wa afya wa hospitali hiyo.
“Ninashukuru sana kwa Ujio wa
Marafiki zetu kutoka Nchini Marekani katika vyuo mbalimbai ambapo wamekuja
maprofesa, maktari, walimu na wauguzi wanafunzi kimsingi wamekuja kujifunza kwa
upande wetu wa Afrika lakini kama hospitali ya JK ambayo ni hopspitali binafsi
wametusaidia kuleta uzoefu wa utaalamu na vifaa vingi tumepokea na ni vya
kisasa vya Upasuaji.” Amesema Dkt. Kyaruzi.
Dkt. Kyaruzi ameeleza mafanikio ya
utoaji huduma za afya katika hospitali hiyo, zikiwa ni huduma bora za kiafya
kwa wakazi wa kigamboni na Dar es Salaam kwa ujumla kutokana na vifaa walivyopokea
kutoka Marekani.
“Vifaa vitasaidia kuongeza utoaji wa
huduma na kuboresha huduma katika Hospitali yetu ya JK, Ninaamini wananchi
wengi watapata huduma bora, tunaomba mahusiano yetu yaendelee kudumu na
yaendelee kuwepo mwaka hadi mwaka ili tuendelee kuwasaidia wananchi wetu
watanzania wanaohitaji huduma bora za afya.” Ameeleza Dkt. Kyaruzi.
Vile vile, Dkt. Kyaruzi amewashukuru
wote wataalamu wa afya wa hospitali hiyo na wale kutoka nchini Marekeni kwa
moyo wao wa kujifunza na kubadilishana ujuzi ili waendelee kutoa huduma bora za
kiafya kwa wananchi.
‘’Kipekee ninawashukuru wote kwa
kuweza kufika katika kubadilishana uzoefu na ninaimani kwa mjumuiko huu wa
wataalamu kutoka taasisi na hospitali mbalimbali tutahakikisha huduma hizi
tunazitoa kwa viwango vya hali ya juu zaidi”. amesema Dkt. Kyaruzi
Mkurugenzi wa Programu ya KIIS Prof. Wiliam Mkanta amesema toka mwaka 2011 kila
mwaka wanakuja wanafunzi tofauti tofauti wakiwa ni wauguzi, madaktari, na wale
wa elimu ya Afya
“Wote wanahusiana na masuala ya afya
na progamu hii huleta wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Marekani na ni wanafunzi
kutoka katika fani ya afya ya jamii, ambao huja kwaajili ya masomo ya muda
mfupi kuanzia mwezi wa sita ,saba na nane” Amesema Prof. Mkanta.
Prof. Mkanta ameongeza kuwa wakati
wanafunzi hao wanakuja kujifunza upenda kutembelea maeneo tofauti tofauti hapa
nchini nan chi zingine za Afrika hii pia inakuza utalii.
“Wanaokuja Nchini Tanzania na
tunakuwa tunakaa wiki nne zinakuwa za mafunzo ya vitendo nakutembelea maeneo
ambayo ni maarufu ya nchini na kama sasa hivi tupo Mwanza kujifunza tamaduni za
watu wa Tanzania, pamoja na nyanja za kiafya, huduma zakijamii kwa kuifata
Jamii kwenye maeneo yao” Ameongeza Prof. Makanta.
Naye, Ritha Raymondi amabaye ni mzazi
amesema kuwa alipompeleka mtoto wake kliniki katika hospitali ya JK alikutana
na wanafunzi kutoka vyuo tofauti nchini Marekani waliokuwa katika program ya
afya ya umma mwaka 2025 na kufanikiwa kujua hali ya mtoto na kupata maelezo ya
kina juu ya mwenendo wa afya ya mtoto wake aliyekuwa na areji.
“Kwa kweli nimefurahi sana ujio wa
hawa ndugu zetu kutoka Nchini Marekani na wamesaidia kujua tatizo la mwanagu
ambaye alikuwa akisumbuliwa na Areji na wamenielezea kiundani sana, sababu za
hiyo areji na namna ya kuitibu, kwakweli ujio wao unafaida sana sana sana,
tunashukuru sana kwa ujio wao na kuiomba JK Hospitali isiishi hapa na iweze
kuwaleta tena mara kwa mara asanteni sana” Amesema Ritha.
0 comments: