KKT KUONGEZA UFAULU WA DARASA LA SABA 2017 KIGOMA
Na Magreth Magosso,Kigoma
WALIMU  wanajifunza mafunzo ya uimarishwaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) Mkoa wa  Kigoma wameiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa walimu na  wanafunzi ili kuleta tija katika matokeo ya wahitimu wa darasa la saba.

Maombi hayo waliyatoa juzi katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo ambayo kimkoa yanafanyika katika chuo cha ualimu cha kasulu na kuongeza kuwa licha ya mtaala wa sasa kuwa na mbinu shirikishi za kumuwezesha mwalimu kumuandaa vizuri mwanafunzi serikali  haina budi  kuongeza kasi katika utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu.


Wakizungumza baada ya ufunguzi wa Mafunzo hayo baadhi ya Walimu hao akiwemo Mwalimu, Geogre Jelome alisema mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha Walimu kuwaandaa wanafunzi katika stadi za KKK kwa kumuwezesha Mwanafunzi kumaliza shule akiwa na uwezo wa kujiajili.


" mafunzo haya tumeyafurahia ,kabla hatujapata mafunzo haya ilitupa shida sana kutumia  mtaala wa zamani na wanafunzi walikuwa hawashirikishwi kwa namna yoyote kwa sasa tunauhakika wa kuwafundisha wanafunzi na  kuelewa kwa makini sana nakumaliza shule wakiwa nauwezo wa kujua kusoma na kuandika", alisema Jelome.

Jelome alisema Ilikufanikisha Mtaala huo unafanikiwa ni kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa kuboresha nyenzo za ufundishaji, posho za walimu na Madarasa ya kutosha ilikuhakikisha wanafunzi wanashilikishwa katika mbinu za ufundishaji.

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo kitaifa Mwalimu Richard Ibraimu  alisema wanawajengea uwezo walimu wa shule za msingi hasa darasa la tatu na la nne ,kuwa na mbinu za kufundisha wanafunzi ili,wafahamu haraka kusoma kuandika na kuhesabu  (KKK ).ili kuongeza ufanisi kwa wahitimu darasa la saba.


Alisema mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo ya uimalishaji wa stadi za KKK yaliyofanyika awali kwa mikoa19 ya Tanzania bara ambapo Mikoa saba iliyokuwa chini ya program ya Equipt ukiwemo Mkoa wa Kigoma haikupata mafunzo hayo, Serikali kupitia WyEST pamoja na OR-TAMISEMI imeona ni muhimu sasa kwa mikoa hii kupewa mafunzo hayo ilikuhakikisha kuwa kunakuwa na mfanano wa kitaifa.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo katibu tawala mkoa wa kigoma Charles Palangyo aliwataka walimu hao kutumia ujuzi huo ili kuongeza kiwango cha ufaulu na ufanisi wa wanafunzi katika mkoa wa kigoma.


Alisema ,Kigoma ni miongoni mwa mikoa ambayo inafanya vizuri katika matokeo ya Darasa la saba , kidato cha nne na cha sita endapo walimu hao watatumia ipasavyo mafunzo hayo waliyo yapata itasaidia kufanya vizuri zaidi kutokana na wanafunzi wengi wanavipaji .

0 comments: