WATUHUMIWA 326 WAKIWEMO WA DAWA ZA KULEVYA HEROINE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA

Kamanda wa Polisi mkoa wa kigoma Ferdinand Mtui akizungumza na
wandishi wa habari juu ya kukamatwa kwa madawa ya kulevya ofisini
kwake kigoma ujiji jana.


NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

JUMLA ya Watuhumiwa 326 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kigoma kwa makosa mbalimbali ikiwemo wahamiaji haramu 226 ,waliokutwa
na madawa ya kulevya aina ya Heroine na mashamba ya bangi 44, na
mtambo wa kutengeneza pombe ya gongo 54 na mmoja kukutwa na silaha
aina ya gobore.

Akifafanua hayo mbele ya wandishi wa habari jana kigoma ujiji ofisini
kwakwe Kamanda wa Polisi, Ferdinand Mtui alisema kwa kipindi
cha wiki moja katika msako endelevu wa watumiaji na wasambazaji wa
madawa ya kulevya wamefanikiwa kukamata madawa hayo kama ifuatavyo,

Kwa upande wa wilaya ya kigoma mjini walikamata kete  tano za heroine
na bang kete 191 na gramu 10,wakati wilaya ya kasulu walikamata
shamaba lenye ukubwa wa robo heka  na gramu 500 za bang, wilaya ya
Kibondo wamekamata miche 10, Kakonko miche 60 ,kilo moja na gramu 500.

Alisema wamekamata jumla ya lita 300 ya pombe aina ya gongo ambapo
wilaya ya kigoma wamekamata lita 229,kasulu 25, kibondo lita 15, kakonko
lita 31,manyovu lita 15,huku wakishikilia mtambo mmoja wa kutengeneza
pombe hiyo wilayani kibondo na wilaya ya uvinza mmoja amekutwa na
silaha aina ya gobore.

Aidha aliwapongeza wananchi kwa kutambua umuhimu wakutoa tarifa ya
uwepo wa wahalifu na wahamiji haramu wenye historia ya uhalifu hasa
wanaotoka  nchi ya burundi na kuwasisitiza wananchi wasiogope kutoa
tarifa zenye maslai mapana ya taifa lao.

Kamanada Mtui alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazowakabili mara tu ya upelelezi kukamilika ambapo kwa sasa
wana kesi moja ya heroine,kesi 8 wahamiaji haramu,kesi 12 pombe ya
gongo,bhang kesi 9 na silaha kesi mojatu.

0 comments: