ZAIDI YA WATU 3,000 KUNUFAIKA NA KILIMO CHA SUNGURA MKOANI KIGOMA

NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

 IMEFAHAMIKA kuwa, zaidi ya wananchi 3,000 mkoani hapa wanatarajia kuodokana na umaskini wa kipato, kutokana na ufugaji wa sungura baada ya kujiunga katika kilimo cha biashara. Hayo yalibainika juzi kigoma ujiji kwenye mkutano wa wafanyabiashara wadogo na wananchikwa ujumla ,ambapo wananchi waliowengi wamehamasika kuingia katika kilimo cha ufugaji wenye tija wa zao la sungura ambalo lina mnufaisha mkulima na taifakwa ujumla. Akielezea hilo Meneja wa Kilimo Biashara wa Namaingo Business Agency, Pascla Stephano alisemaviongozi wa taasisi hiyo wamethubutu kuwapatia uelewa wa kukuza sekta ya kilimo chenye tija kwa wananchi wenye uthubutu wa kutoka katika dimbwi la ufakiri wa kipato ambapo kupitia tasisi hiyo itasimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa hiyo. Alisema fursa ipo kwa wakazi wa kigoma kuondokana na umaskini wa kipato endapo watashiriki katika shughuli za kilimo biashara chenye tija kwa kuwa rasilimali za mkoani hapo zina mashiko kwa jamii hasa ardhi zenye rutuba ambazo hazitumiwi ipasavyo kutokana na kulima kimazoea. Alisema kuwa baadhi ya wananchi wameonyesha namna ambavyo,wataitumia fursa hiyo kwa kuanzisha ufugaji wa sungura kibiashara,mradi ambao una soko la uhakika ndani na nje ya nchi kwa kuwa una faida kubwa kwa wanaofanya ufugaji huo. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Namaingo Business Agency,Biubwa Ibrahim alisema Watanzania wengi,wamekuwa waoga katika kutumia fedha ili,wajiajiri wenyewe na hulazimika kutumia fedha nyingi katika masomo ili wajiriwe serikalini kitendo kinachoongeza utegemezi wa kipato. Biubwa alielekeza kuwa kilimo ndiyo sekta pekee inayoweza kutumika na kuwaondolea wananchi umasikini ,iwapo watafanya kilimo chao kuwa chakibiashara huku akiri wengi kutokujua eneo sahihi la kupewa ushauri na mawasiliano na sekta zingine,ili kuwaelimisha ubora wa bidhaa inayohitajika katika soko la uhakika la ndani na nje.

0 comments: