WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA HISTORIA YA DR.LIVINGSTONE-KIGOMA


NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma wamehamasishwa  watunze  na kuhifadhi mazingira sanjari na kutembelee kituo cha mambo ya kale Cha Dkt,LivingStone kilichopo Kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma Ujiji,ili jamii itambue thamani ya rasilimali hiyo inayowapa mwanga wa kutambua tamaduni zao katika karne ya 18 na 19. Nyakati za ukoloni.


Hayo yalisemwa jana katika uzinduzi wa vikundi mbalimbali vya wanafunzi kwenye manispaa ya ujiji uliolenga kuwaelimisha umuhimu wa uhifadhi wa hifadhi za taifa ambazo zitalindwa na vijana kwa kuhamasisha jamii dhidi ya kutembelea vivutio vya kale vilivyopo mkoani kigoma hasa historia ya ujio wa Dtk.David Livingstone na biashara ya utumwa kwa kuona masalia ya zana mbalimbali zilizotumika nyakati hizo.

Akithibitisha hilo, Mwenyekiti wa Tasisi ya Vijana Tanzaleo Lubatuka Japheth alisema changamoto ya uwindaji haramu wa wanyama katika hifadhi za taifa ni janga kwa kizazi cha leo na kesho hali iliyopelekea tasisi hiyo kutembea kila eneo lenye historia ya uhifadhi wa kale kufikiwa ,ili vijana wawezeshwe kielimu kwa kufika katika makumbusho husika,ili wahamasishe utalii wa ndani ya mikoa yao.

Alisema uingizwaji wa mifugo katika hifadhi za taifa ni kukiuka sheria za kuwalinda wanyama pori na uoto wa asili ambao upo kwa ajili ya kulinda mazingira kwa wakati tulionao  na siku za usoni na kuhimiza vijana watumie fursa hizo kwa kuunda vikundi vya uhamasishaji wa uhifadhi mazingira kama sehemu ya ajira pia kuongeza pato la taifa kwa fedha za kigeni.

Kwa upande wa Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Dkt,Livingstone Miriam Mkonya aliongeza kwa kusema wananchi wa hapo hawana mwamko na hawajui umuhimu wa utalii wa ndani ingawa serikali imeweka kima cha chini cha fedha sh.2,000 kwa wakubwa na watoto walio chini ya miaka sita ni bure na zaidi ya miaka saba watapata historia ya hapo kwa sh.1,000tu.

Naye Maimuna Samata ni miongoni mwa wanafunzi watakaopata fursa ya uhamasishaji kutoka shule ya sekondari ya kitongoni alisema uharibifu wa mazingira wa hifadhi za taifa na uwindaji haramu ni moja ya sababu ya kupoteza mapato ya serikali na kupoteza uhalisia wa hifadhi hizo na kuwaomba wananchi watambue idara ya mambo ya kale kwa kutembelea vituo vilivyopo ndani ya mikoa yao.

0 comments: