BURUNDI FICHUENI WAHALIFU, DC KANAL GAGUTI-BUHIGWE





   NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma Kanali Marco Gaguti ameomba Uongozi wa Serikali ya Nchi ya Burundi , itoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wa hapo, kwa kuwabaini  wahalifu wa  nchini humo wanaojipenyeza na kupata hifadhi  katika kambi za ukimbizi za hapa kwa kuogopa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalibainika hivi karibuni katika kikao cha majadiliano baina ya Kanali Gaguti na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, Niyomkuru Laetitia alipokuwa  akimuhoji   sababu ya ongezeko la wahamiaji  2230 kwa kipindi cha Januri , mwaka huu wakidai wanakimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama tawala kinacho julikana kama  ` IMBONELAKULE’ .

'' leo nimetembelea vituo na kuona ongezeko kubwa  la waomba hifadhi ya ukimbizi,lakini  maelekezo mapya yametolewa na serikali kwa  kutambua  sababu za msingi ili apate hifadhi, hakuna kuingia kwa makundi bali kuchunguzwa tarifa za kila mkimbizi kwa wakati wake ili kuepuka wahalifu wanaotumia fursa ya ukimbizi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ushirikiano katika taarifa za wahamiaji    kabla ya mambo kubadilika ,ili tuchukue  tahadhari  kwa faida ya  wote" alisema kanali Gaguti.

Akijibia hilo Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba (Musitanteri) Niyonkuru Laetitia alisema kwa sasa nchi ya Burundi ni tulivu na wanaokimbia nchini  mwao ni wale wanaokimbia njaa na wengine kukimbia uhalifu aliofanya nchini Burundi na  kuomba hifadhi  na  waliorudishwa Burundi kipindi cha nyuma na wengine  wanapenda  kupelekwa Nje ya Nchi za Amerika na Ulaya kwa madai ya kuwafuta ndugu na jamaa zao waliopelekwa huko .  

Laetitia akiri uongozi wa hapa kabla ya kuwapokea wachunguze vitambulisho vyao,ili kubaini wahalifu wanaokimbia kujibu tuhuma nchini mwao badala yake hutumia kigezo cha machafuko ilihali wanakimbia kujibu kesi za uhalifu na wengine hutumia ukimbizi ili kuongeza nguvu ya kwenda kuipindua serikali iliyopo na kuomba Tanzania iwakabidhi pindi itakapogundua hila hizo.

Nizigimana Silivesta ni Mmoja ya  waomba hifadhi kutoka Burundi, alisema kinachowakimbiza  Nchini mwao ni usalama  mdogo hasa  vikundi vya watu wahalifu huwatisha kutokana na baadhi ya ndugu zao walioikimbia nchi hiyo wanaipinga serikali husika.

0 comments: