BITEKO AZIASA BENKI KENDELEA KUDHAMINI MAONESHO YA WAFUGAJI KIBIASHARA

  
Na Mwandishi wetu, Michuzi Tv
NAIBU Waziri Mkuu Dotto Biteko ametoa wito kwa Wadau wezeshi wa wafugaji nchini kuendelea kutoa elimu na mikopo ili waweze kufuga kibiashara wapate tija katika ufugaji wao.

Amewataka wadau wezeshi hao kutoishia kwa wafugaji wa kibiashara bali wawafikie wafugaji wa kienyeji ili na wao waweze kuwa wafugaji wenye tija nchini kwani hilo ndilo lengo la serikali ya awamu ya sita ambayo inalenga kuwanyanyua wafugaji.

Naibu Waziri Mkuu Biteko amesema hayo leo Juni 16 wakati akifunga maonesho hayo ya siku tatu ambayo yamefanyika Ubena Zomozi ,Halmashauru ya Chalinze Mkoani Pwani.

Naibu Waziri Mkuu amefunga maonesho hayo akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amepata udhuru , hivyo natoa wito huu kwa uongozi wa Benki zulizo toa udhamini huu ambazo ni Benki ya Kibiashsra ya Kilimo TADB na NMB kundelea kutoa elimu kwa wafugaji kwani wao wamekuwa wakichangia migogoro na wakulima kutokana na kwenda kulisha mifugo yao kwenye mashamba.

"Halmashauri za wilaya nchini zitunze maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo"

Serikali itaendelea kuunga mkono maonesho ya Wafugaji wa Kibiashara nchini ili waendeleze haya maonesho ambayo yanatoa elimu na kutoa Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara utakaoongeza tija kwa wafugaji na kupata soko katika soko la kimataifa.

"Maonyesho haya muyapeleke katika ngazi za Kanda ambako yatakutana walengwa ambao ni wafugaji wa kienyeji na wawape elimu wabadilike na kufuga kibiashara".

"Wafugaji wanapitia changamoto nyingi hivyo hivyo msichoke kuwapa elimu ya ufugaji wa Kibiashara nina imani watabadilika taratibu na badaye nchi itakuwa na wafugaji wenye mifugo yenye faida.

"Msiwasahau wafugaji wanaofuga kienyeji na mwakani naomba baadhi wawepo kwenye maonesho haya kwani watakapokuja watajifunza na kubadilika"amesema Biteko.

Wakati huohuo amewaonya wafugaji kuacha migogoro na wakulima na kuacha tabia ya kupitisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima huku akiwasisitiza elimu itumike pamoja na sheria katika kumaliza migogoro hiyo.

"Hivi sasa dunia inakwenda kidigitali hivyo hatakwa sisi ambao tulilelewa katika familia za wafugaji nawaasa mbadilike msiwe kama wafugaji wa zamani ambao walikuwa wakifuga na kulalia ngozi lakini wafugaji wa kisasa wanalalia magodoro hivyo nanyi mbadilike sasa mfuge mifugo itakayowaletea tija acheni kufuga kizamani" amesema Biteko.

Akiwa katika banda la Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini TADB akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB David Nghambi amesema kuwa Benki hiyo kipindi cha miaka mitatu wametoa mikopo ya zaidi ya Bil.13, wamewawezesha wafugaji kibiashara ili wawe na uhakika wa masoko kimataifa kwa kunenepa mifugo, pia wametoa mikopo ya bilioni 47 kwa wafanyabishara wa maziwa.

Aidha akikagua banda la NMB Mheshimiwa Biteko amezindua huduma ya Bima kwa mifugo ambayo ni 20,000 kwa mwana na inatoa kinga dhidi ya vifo vya mifugo vitanyotokana na radi, majeraha ya ndani na nje kwenye eneo la usafiri, moto, dhoruba, kung'atwa na nyoka mafuriko, magonjwa ya asili na yasiyodhibitika kwa mifugo.

0 comments: