JKCI YASHIRIKI KAMPENI YA AFYA CHECK KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO

  

   Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila akizungumza hivi karibuni na wananchi (pichani hawapo) waliojitokeza kwenye uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam linalofanyika katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam, lililoratibiwa na Afyacheck. JKCI yashiriki kampeni ya afya check kutoa huduma za matibabu ya moyo

   Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila akikata Utepe hivi karibuni kuashiria uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam linalofanyika katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam.

  Afisa Muguzi msaidizi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Feliciana Mselle akimpima shinikizo la damu Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mlangwa Yango akizungumza na mwananchi aliyejitokeza hivi karibuni wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam linalofanyika katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam.

   Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Agnes Ndangamila akizungumza na mwananchi aliyejitokeza hivi karibuni wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam.

   Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila (kulia) akiipongeza Hospitali ya JK wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam likiratibiwa na Afyacheck.

    Wafanyakazi wa Hospitali ya JK wakifurahia kwa kupiga makofi wakati Katibu wa Hospitali hiyo Malieta Mashimba (kulia) alipokuwa akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila juu ya huduma wanazozitoa wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Barafu Mburahati. Zoezi hilo la upimaji wa siku 10 litafanyika katika halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam kwa kuratibiwa na Afyacheck.  (PICHA NA KHAMISI MUSSA)

0 comments: