Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Deogratis Nkya akiwaonesha wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi jinsi wanavyofanya upasuaji wa kuzibua tundu la moyo wa mtoto bila ya kufungua kifua wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI Aprili 21, 2024 kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Dkt. Nkya ni makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Jimbo la Kigamboni.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi aina za upasuaji wa moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo wakati kamati hiyo ilipotembelea JKCI kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni misimamizi wa wodi ya watoto Theresia Marimo akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi huduma za matibabu ya moyo wanazozipata watoto waliolazwa katika wodi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaongoza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi kwenda kuona ujenzi wa jengo la utawala na vipimo unavyoendelea. Kushoto kwa Mkurugenzi ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni na kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt.Godwin Mollel.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
0 comments: