NMB YACHANGIA MILIONI 100.9 VIFAA VYA ELIMU NA AFYA RUVUMA

BENKI ya NMB imetoa shilingi milioni 100.9 ili kusaidia maendeleo katika

sekta za afya na elimu mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Faraja Ngingo
kwenye hafla ya kukabidhi madawati kwa shule za msingi Manispaa ya
Songea iliyofanyika katika shule shule ya msingi Kiburang’oma ambapo
mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.

Ngingo amebainisha kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi milioni 24
zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa vitanda na magodoro katika hospitali ya
Halmashauri ya Madaba na shilingi milioni tano zilitumika kutengeneza
madawati 50 katika shule ya sekondari Matetereka.

Kulingana na Meneja huyo, shilingi milioni 33.7 zilitolewa katika Wilaya ya
Nyasa kwa ajili ya ununuzi wa mabati katika shule za
Lundo,Chinula,Limbo,Ndingine,Chiwindi na Nangombo.

Ameongeza kuwa NMB pia imetoa shilingi milioni 22 katika wilaya ya
Songea kwa ajili ya kutengenezea madawati 220 katika shule za msingi
Legele,Kiburang’oma,Lipupuma,Londoni na Mkuzo.

Ngingo amesema NMB imenunua bati 150 zenye thamani ya shilingi
milioni 5.25 kwa ajili ya shule ya msingi Ntungwe wilayani Namtumbo na
kwamba NMB imetoa shilingi milioni 10.2 kwa ajili ya vifaa vya hospitali ya
wilaya ya Tunduru.

“Sisi kama wadau tunawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo
kwa kusaidia jamii,tulipopata maombi haya ya kuchangia maendeleo ya
elimu ,tuliamua mara moja kuja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya
maendeleo’’,alisisitiza Meneja wa NMB.

Hata hivyo amesema kwa miaka kadhaa NMB imekuwa ikisaidia miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Ruvuma kwa kujikita zaidi katika miradi
ya elimu kuchangia madawati na vifaa vya kuezekea na kwenye afya
kuchangia vitanda,magodoro na vifaa vingine vya matibabu.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza NMB kwa msaada huo
mkubwa kwa wananchi wa Ruvuma.

Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amejenga miundombinu mingi
ya elimu na afya hivyo wadau wengine kama NMB wanapojitokeza
kuchangia vifaa kwenye miradi hiyo wanaunga mkono moja kwa moja
juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.

Ametoa rai kwa wadau wengine mkoani Ruvuma kuiga mfano wa Benki ya
NMB katika kuchangia maendeleo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile
ameishukuru NMB kwa kupunguza changamoto ya madawati na meza
katika shule za msingi na sekondari Manispaa ya Songea.

Amebainisha kuwa katika shule za msingi zilizopo Manispaa ya Songea
kuna upungufu wa madawati 5,863 na katika shule za sekondari za
Manispaa ya Songea kuna upungufu wa meza 6,600.

Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kiburang’oma Mary Komba
na John Haule kwa niaba ya wanafunzi wenzao wameishukuru Benki ya
NMB kwa Msaada wa madawati 40 ambayo yamepunguza uhaba wa
madawati.

Benki ya NMB imezifikia wilaya zote nchini ikiwa na matawi zaidi ya
230,wakala zaidi ya 20,000 na wateja zaidi ya


0 comments: