UWEPO WA VIWANDA UTACHANGIA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA KILIMO-MHANDISI STELLA MANYANYA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:02 PM
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
NAIBU
Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya
amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji
wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la
uhakika.
Mhandisi
Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa kongamano
la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini
lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).
Amesema
ili kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta
binafsi na Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara."Tasisi
za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za
ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili
kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema.
Mhandisi
Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi
kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha
wawekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani.
“Kuna
changamoto kadhaa katika taasisi za fedha ambazo ni lazima zifanyiwe
kazi kwa sababu wafanyabiashara wengi wanapokopa fedha kwa mfano kununua
mashine wanatumia muda mrefu kutafuta ushauri. Niwaombe kuwasaidia
kuwapa ushauri pale mnapowakopesha,"amesema Mhandisi Manyanya
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),
Geofrey Simbeye, ameishauri Serikali kuanzisha benki maalumu
zitakazosadia kutoa mikopo ya kuanzisha na kuendeleza viwanda kama
imekusudia kufikia uchumi wa kati unaotegemea sekta hiyo.
Pia
Simbeye amesema licha ya ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuonesha
Sh. trilioni 16.3 zilitolewa kwa sekta binafsi ni alisimia 9.8 tu ya
fedha hizo iliyoelekezwa sekta ya uzalishaji huku kiasi kikubwa
kikielekezwa kwenye biashara.
“Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CRDB, Charles Kimei, amezungumza mambo mengi, lakini
ninachosisitiza ni lazima tuwe na mfumo mpya, kwa sababu kama fedha
zilizokopeshwa kwa private sekta ni Sh.trilioni 16.3, kwa mujubu wa
taarifa ya BoT.
“Na
ripoti ya Benki Kuu hiyo hiyo, inaonesha katika hizo ni asilimia 9.8 tu
ndizo zimekwenda kwenye viwanda. Sasa tunajiuliza kwa ‘rate’ hiyo
tutafika kwenye viwanda? Amehojia Simbeye.Amesema
benki za kibiashara zimekuwa zikiangalia zaidi wapi zinapata faida
ambapo mikopo inaweza kurudi haraka, ambapo mikopo mingi imekuwa
ikielekezwa kwenye biashara ambako watu wengi hukopa ili kuagiza bidhaa
za biashara na kujenga nyumba tofauti na uwekezaji wa viwanda ambao ni
wa muda mrefu.
“Sasa
tunajiuliza swali je, tutaendelea kutegemea benki hizi za kibiashara
katika kuendeleza viwanda hapa Tanzania? Tunatakiwa kufikiria nje ya
boksi nini tufanye.
“Kujenga
uchumi wa viwanda nchini Tanzania ni sawa sawa na projecti ya kitaifa
yaani ni project ya kujenga Taifa ndiyo itakayotulepeka kwenye uchumi wa
viwanda na kama tunaichukua kama project ya kitaifa lazima tuje na
mfumo tofauti wa kuiwezesha,” amesema Simbeye.
Amesema
mchakato wa ujenzi wa viwanda unapaswa kuchukuliwa kama unavyochukuliwa
mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge)
ambapo Rais amesema anazo zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3.5 za
kujenga mradi huo kuanzia Dar es Salaam hadi makao makuu ya nchi Dodoma.
Amesema
hivyo ni vema kuwa na chombo maalumu kitakachokuwa kikitoa mikopo ya
maendeleo hasa sekta ya viwanda ili kuwezesha kufikia lengo la uchumi wa
kati unaotegemea viwanda.“Hakuna
kiwanda kinaanzishwa kikae miaka mitano, kiwanda ni project za milele
na milele, wewe mwanzishaji utakufa lakini kile kiwanda kipo, kwa hivyo
vinahitaji uwekezaji wa muda mrefu.
“Tatizo
hapa wanaangalia faida zaidi lakini tukiwa na ‘industrial development
bank’ kama TIB ni kama una-empower watu kuanzisha viwanda,” amefafanua
Simbeye.Ameongeza
sensa ya maendeleo ya viwanda ya mwaka 2013 iliyozinduliwa mwaka 2016
inaonesha Tanzania ina jumla ya viwanda 49,242 lakini viwanda vikubwa ni
1,322 tu. "Hivyo ni vema kujiuliza kwanini viwanda vidogo ndiyo vingi
na kwanini visianzishwe viwanda vikubwa".
Amesema
tatizo kubwa ni ukosefu wa mitaji, hivyo ni vema kusaidia kuanzishwa
viwanda vingi vikubwa vitakavyosaidia pia kuanzishwa kwa viwanda vidogo
vitakavyokuwa vinazalisha malighafi kwa za viwanda vikubwa na kutoa
ajira nyingi kwa wananchi.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Mabenki ya Tanzania, Dk. Charles Kimei, amesema licha ya
taasisi za fedha kuwa na jukumu la kusaidia upatikanaji wa fedha kwa
watu bado kuna changamoto nyingi nchini ikiwamo wafanyabiashara wengi
wazawa kutoaminika katika taasisi za fedha hususani za kigeni.
Dk.
kimei amesema kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wajasiriamali
wadogo na wa kati taasisi za fedha nchini zinapaswa kuongeza
ushirikiano na wajasiriamali hao badala ya kufikiria viwanda vikubwa tu.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere(MNMA) kuhusu wajibu wa taasisi za fedha katika
kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi
wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles
Kimei akichokoza mada wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za
fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tasisi ya Sekta Binafsi Nchini(TPSF),Geoffrey Simbeye,
akichokoza mada wakati wa kongamano la kujadili umuhimu wa mabenki na
sekta binafsi katika maenedeleo ya Viwanda.
Naibu
Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dr.Thomas Ndaluka
akitoa neno kwenye Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika
kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mhadhiri
wa Chuo Cha MNMA, Binto akitoa mada ya Ujasiliamali ktika Uwekezaji wa
Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Mkurugenzi
wa Uchumi ,Utafiti na Sera , Benki kuu ya Tanzania Johson Nyela
akichangia jambo wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha
katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akiwa ameketi pamoja na Washiriki
wengine wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza
Viwanda Tanzania.
Mkuu
wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof Shadrack Mwakalila wa
kwanza kulia akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,
Mhandisi Stela Manyanya (Katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB
Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya wakati wa
Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda
Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: