CHAMA CHA WAFANYAKAZI (TUGHE) MKOA WA DAR ES SALAAM CHAPATA MWENYEKITI MPYA


Mwenyekiti mteule wa Chama Cha Wafanyakazi mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda  Chimwege (kushoto) akionesha chati cha ushindi kwa wajumbe mara baada ya kukabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi Emmy Rweyendela kulia baada ya kuwabwaga wenzake wanne, uchaguzi uliofanyika Oktoba 20, 2017 Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHMISI MNUSSA)
Msimamizi wa uchaguzi Emmy Rweyendela (kulia) akitangaza matokeo mara baada ya kupatikana mshindi

  Katibu (TUGHE) mkoa, Gaudensi Kadyango alianza kwa kuwashukuru wajumbe kwa kazi nzuri ambayo wameifanya na pamoja na madongo lakini napenda kuwahakikishia ni moja ya kipimo cha uongozi na ninjia ya kutaka kufikia malengo , alisema Kadyango.

Pamoja na kutaka kumtoa Katibu anaye ongea lakini najua ni changamoto za kazi lakini nitaendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano mkubwa na pia naomba haya yaliyoongelewa hapa yaishie hapahapa na mimi nipo na moyo mweupe na ninajua ni mambo ya kazi, aliendelea kusema.

Napenda niwahakikishie kwamba mimi ni mkomavu na niwatowe hofu nipo pamoja na ninyi kwa moyo mweupe na msisite kwa lolote na ninajuwa nichangamoto ya kupenya katika kufika mtu anapopataka kufika.

Napenda kuchukua fulsa hii ya kumpongeza Mwenyekiti mteule na kukuhakikishia sisi makatibu wa mikoa na wajumbe hawa tunakupa ushirikiano wa kutosha ili ufikie malengo yako na tuanzie kwenye matawi na kama sisi wenyewe kama viongozi.

Ndugu wajumbe na omba tuwe mfano kwa kuanzia katika matawi na utaongoza mikoa mitatu nayote utahakikisha unatimiza wajibu katika mikoa hiyo  alisema Kadyngo


 Mwenyekiti Kamati ya Wanawake (TUGHE) Taifa, Dokt. Jane Madete (kushoto) aliomba kumpa ushirikiano Mwenyekiti huyo kutoka katika  Kamati tendaji matawi, mikoa na hata ngazi ya Taifa kwa yale yatakayohusu mikoa na tunakupongeza sana
Mwenyekiti mteule  mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda  Chimwege akizungumza jambo mara baada ya kuchaguliwa kukiongoza Chama hicho kwa miaka mitano
Msimamizi wa uchaguzi, Emmy Rweyendela (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi  Mwenyekiti mteule  mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda  Chimwege katikati na kushoto ni Katibu (TUGHE) Mkoa, Gaudensi Kadyango

Mwenyekiti mteule Mziwanda Chimwege (wa pili kulia waliokaa)  katika picha ya pamoja na wajumbe


Baadhi ya wagombea waliokosa kinyanganyiro hicho , Almas Mzee amempongeza Mwenyekiti huyo mpya na kuahidi kumpatia ushirikiano ili kuleta tija.

 Mwenyekiti mteule akizungumza na waandishi wa habari (pichani hawapo) alisema Namshuru Mungu kwa nafasi hii kutokana na  usimamizi bora wa sera nilizo jipangia ambazo  zitakazomlinda  mfanyakazi, pamoja  na kufufua matawi ngazi za mkoa  ili kutetea masilahi  ya wafanyakazi na watumishi ndani ya chama. Ameongeza kuwa  uwazi wa matumizi na mapato ya fedha utakuwa wa usawa ili kumlinda mtumishi  katika kazi kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa sera yake ya HAPA KAZI

0 comments: