RPC MKOA WA KIGOMA AONYA WAKIMBIZI


Na Magreth Magosso,Kigoma

KAMANDA wa Polisi Mkoaa wa Kigoma Ferdinand Mtui ametoa mwito kwa wakimbizi wanaoishi katika kambi za mkoani humo,wasalimishe silaha  kwa viongozi wao kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za Tanzania ,ili kutii sheria bila shuruti.

Akifafanua kauli hiyo mbele ya majira DCP Mtui alisema  awali alitoa siku tatu kwa wakimbizi wasalimishe silaha kwa mujibu wa sheria mtambukwa kwa lengo la kupunguza utunzaji wa silaha kinyume cha sheria,ambazo hutumika katika matukio ya kihalifu mkoani humo.

Alisema  kupitia mkakati waliouweka na viongozi wa wakimbizi wakiwemo sungusungu na viongozi wa kambi za mtendeli,nduta  na nyarugusu juu ya msako endelevu wa kubaini wahalifu na silaha haramu unaolenga kwenye vijiji vinavyozunguka kambi hizo na mapori makubwa yanayozunguka barabara kuu ya  kigoma hadi wilayani Kakonko .

“niliagiza wakimbizi wanaomiliki silaha nyepesi za kivita na ndogondogo wazisalimishe kwa viongozi wao,kwa nia ya kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi kutokana na kuzagaa hovyo kwa silaha hizo kinyume cha sheria ya taifa husika.

Alieleza kuwa tamko hilo lilichangia Machi,9,mwaka huu,saa 3.00 katika kambi ya nduta wilayani kibondo askari wakiwa katika doria walifanikiwa kuipata   silaha  moja aina ya SMG isiyokuwa na magazine wala  risasi yenye namba   66-20148294 iliyokuwa imetelekezwa katika pori lililo karibu na kambi hiyo.

Aliongeza kwa ksuema mchakato unaendelea kuwapata wahusika waliotelekeza silaha hiyo,ili sheria ifuate mkondo wake na kuwasihi wananchi watoe tarifa za wahalifu ili,kukomesha matukio ya utekaji mabasi ya abiria na mauwaji wa raia wasio na hatia.

0 comments: