Huyu ndiye mwanamke aitwaye Fatuma Issa 22 Mkazi wa Kijiji cha Isengule Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi akiwa katika chumba maalumu katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda baada ya kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja ambapo alijifungua watoto hao hapo machi 12 katika Hospitali hiyo kati ya watoto hao mmoja ni wakike na watatu ni wakiume.
Picha Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
MKAZI wa kijiji cha Isengule , mwambao mwa Ziwa Tanganyika katikawilaya ya Tanganyika mkoani Katavi , Fatuma Issa (22) amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda mwishoni mwa wiki.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo , Alexanda Kasagula alisema mama huyo alijifungua watoto hao wanne mwishoni mwa wiki kwa njia ya kawaida ambapo mama na watoto wake hao wote wakiwa na afya njema.
“Mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 800 ,mtoto wa pili alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 500 , watatu alizaliwa akiwa na uzito wa kilo moja na gramu 800 huku wanne alizaliwa akiwa na kilo moja na gramu 700.
Kati ya watoto hao watatu ni wakiume hali ya mzazi na watoto wake wote wanaendelea vizuri bado wamelazwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapa “ alieleza .
Kwa upande wake , Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jafar Kitambwa alieeleza kuwa mama huyo na watoto wake wataendelea kuwa chini ya ungalizi hospitalini hapo hadi hapo watakaporuhusiwa rasmi kwenda nyumbani
“ Mie na mume wangu sasa tuna idadi ya watoto watano uzazi wangu wa kwanza nilizaa mtoto mmoja ambaye yuko hai.Hii itakuwa mara yangu ya pili kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika uzao wangu wa pili nilijifungua mapacha lakini mmoja wao alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa na pacha mwenzake alikufa miezi mitatu baada ya
kuzaliwa.
Nimejifungua watoto wanne lakini tangu nijifungue sijapata tatizo lolote la kiafya naendelea vizuri mie na watoto wangu wote nawashukuru wauguzi ambao wamenisaidia hadi nimejiufungua salama bila ya matatizo yeyote yale “ alieleza Alieleza kuwa mama yake mzazi ndie anayemwangalia hospitalini hapo huku akimsadia kuwalea watoto hao .
0 comments: