POLISI 40 WAUAWA KASAI DRC

mediaBaadhi ya wapiganaji wa zamani wa wakiwasili KanangaRFI/Sonia Rolley
Kundi la wapiganaji wa Kamwina Nsapu nchini DRC limetekeleza mauaji ya maafisa 40 wa polisi katika shambulizi jimboni kasai,maafisa katika eneo hilo wamearifu.
Shirika la habari la Uingereza BBC Limeripoti kuwa wapiganaji wa kundi la Kamwina Nsapu walishambulia msafara wa maaskari hao.
kiongozi wa Kasai Francois Kalamba ameeleza kuwa askari sita waliachiwa huru lakini wengine walichinjwa.
Machafuko katika jimbo la Kasai yalianza mnamo mwezi August mwaka jana baada ya vikosi vya usalama kumuua kiongozi wa kundi hilo la Kamwina Nsapu.

0 comments: