MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YALIYO FANYIKA KATIKA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI


Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani katika kuadhimisha siku hiyo

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo, Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo.
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo, Puyo Nzalayaimisi akipongezwa na Mkurugenzi wa kituo cha  People With Drugs Dependence Relief  Foundation (Pedderef),  Nuru Salehe  mara baada ya kuzungumza
 Jacqueline Samson, akizungumzia historia yake na kufanikiwa kuacha madawa hayo ya kulevya akiwa kituoni hapo na akatumia nafasi ya kumshukuru, Mkurugenzi wa kituo hicho na kusema hakika ujio wenu umekuja muda muafaka na karibuni tena na mzidi kuongea na wahisani ili tuwezeshwe na tujikwamue na maisha haya kwani tuna watoto wanasoma na tuna famila zinatutegemea, alisema kubwa hata tukiacha kama unavyofahamu Mgeni wetu mara baada ya hapa tutakwenda wapi? kama unavyojuwa familia zetu hali zao, kubwa tuwezeshwe kipesa tuachane na utegemezi na mwanaume atakushawishi na ukibeba mimba anakutelekeza na hata senti tano hakusaidii, hapa nilipofikia ninajitambua na ninajutia kuupoteza musa wangu katika mambo haya.
Jacqueline

 Ashura Diwani akizungumza jambo
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo, Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo cha  People With Drugs Dependence Relief  Foundation (Pedderef),  Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika Dar es Salaam juzi . Kulia ni Jacqueline Samson na Ashura Diwani. ambao wanaonufaika na huduma inayotolewa na Kituo hicho ambacho kinapambana kunusuru watumiaji wa Dawa za Kulevya
Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema, napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliojitolea na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hicho kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuipata kituoni hapo

0 comments: