JAPAN: NI LAZIMA TUJIANDAE KUKABILIANA NA MASHAMBULIZI TARAJIWA YA KOREA KASKAZINI


Waziri wa zamani wa Ulinzi Japan ametaka kuimarishwa uwezo wa kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi tarajiwa ya Korea Kaskazini.
Itsunori Onodera, Waziri wa Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Japan ambaye kwa sasa ni mkuu wa Baraza la chama tawala nchini humo, amesema kuwa, harakati zozote za kijeshi za Korea Kaskazini dhidi ya Japan, zitakabiliwa na jibu mbadala. Matamshi hayo yamekuja kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Pyongyang ya kuvurumisha makombora manne katika maji ya Japan.
Itsunori Onodera, Waziri wa Waziri wa zamani wa Ulinzi Japan
Duru za habari zinaeleza kuwa, viongozi wa Tokyo wamekusudia kuchukua hatua kali katika sera za kiulinzi katika kukabiliana na hatari dhidi yake. Moja ya mambo yanayowatia wasi wasi mkubwa viongozi wa Japan ni kwamba, mwezi uliopita, Korea Kaskazini iliboresha zaidi mfumo wa mafuta ya kuchochea makombora yake kwa kuufanya kuwa mgando. Kabla ya hapo Pyongyang ilikuwa ikitumia mafuta laini katika shughuli za ufyatuaji makombora.
Sehemu ya makombora ya jeshi la Korea Kaskazini
Hatua ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini kufyatua makombora yake manne katika maji ya Japan, iliifanya Washington kutuma nchini Korea Kusini mfumo wake wa ulinzi wa makombora wa THAAD, ambao umekuwa ukilalamikiwa na nchi za China, Russia na Korea Kaskazini. Taarifa iliyotolewa na Pyongyang ilisema kuwa, jaribio lake hilo la makombora ni maandalizi kwa ajili ya kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Japan.

0 comments: