Picha ya Pamoja wanafunzi na walimu baada ya kupokea vitabu |
Diwani
wa Kata ya Kilungule Mh. Saidi Fella leo amepokea msaada wa vitabu vya
kufundishia na kujifunzia kwa wanafuzi wa shule za msingi pamoja na
Sekondary kutoka kwa rafiki zake wa Oxford University Press Tanzania,
Vitabu hivyo vimegawiwa katika shule ya msingi Charambe, Chemchem pamoja
na Kingugi na kwa upande wa Sekondary.
Diwani
Saidi Fella amewashukuru Oxford na kuwasisitiza wanafunzi kusoma
kwabidii kupitia vitabu lakini pia kuvitunza kwa maana ya wadogo zao
waje kuvitumia vitabu hivyo kwa baadae, hata hivyo amewata walimu
kuhakikisha wanavipiga mihuri vitabu ili wanafunzi wanapo azima kwenda
kusoma nyumbani wakumbuke kuvirejesha.
Maria
Mlay kutoka Oxford amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kupitia
vitabu hivyo ili kutimiza ndoto zao katika maisha, lakini pia kuvitunza
vitabu hivyo.
Pia Saidi Fella amewashukuru Oxford kwa mchango huo wa vitabu katika kata
yake na ameendelea kusisitiza wadua kuendelea kumsapoti katika kata yake
ya Kilungule kwani ni Kata mpya na bado inamaitaji mengi zaidi ya
miundo mbinu, Afya pamoja na Elimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: