Baadhi ya waandishi na wageni waalikwa wakifatilia jambo
RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI MIKAKATI NA NJIA SAHIHI ZA KUUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:49 AM
Akifungua
Mkutano wa kujadili mikakati na njia sahihi za kuutokomeza ugonjwa wa
kipindupindu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka
watumishi wa idara za afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia
njia mbalimbali ikiwemo kuvitumia vyombo vya habari ili ugonjwa huo
usiendelee kupoteza maisha ya watanzania wengi.
RC
Makonda ameeleza kuwa tangia ugonjwa huo uliporipotiwa kwa mara ya
kwanza 15 Agosti 2015 idadi ya waathirika imeongezeka na kufikia 5180
huku watu 80 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, hivyo elimu na
uhamasishaji unahitajika ili watu wengi wasiweze kupoteza maisha.
Nakusisitiza
kuwa kampeni ya usafi iwe endelevu kwani usafi unaanzia nyumbani, na
kuwataka watanzania wasiwe na kasumba ya kuona kuwa wakifanya usafi yeye
ndiye anapata sifa kwani suala hilo linatija kwa watu wote, na kuwataka
watumishi hao licha ya elimu waje na mikakati ya kutokomeza kabisa
ugonjwa huo.
Kwa
upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Afya ameitaja Dar es Salaam
kuongoza kitaifa kwa kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa wa kipindupindu
ambapo kuna waathirika 5098 huku vifo vikiwa 47, kiwilaya kwa mkoa huo
ameeleza kuwa takwimu zinaonesha Kinondoni inaongoza kwa kuwa na
wagonjwa 2337 vifo vikiwa 18, Ilala 1804 waathirika na vifo 4, huku
Temeke ikiwa na waathirika 955 na vifo 16, na kupendekeza changamoto za
maji safi na salama zishughulikiwe, uuzwaji holela wa chakula, uwepo wa
taka ngumu.
Pia
muwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Grace Sabuti (wapili kulia)
amesisitiza kuwa uwepo wa takwimu sahihi za ugonjwa wa kipindupindu
utasaidia kuleta suluhisho hivyo ni vyema mamlaka husika ikalisimamia
hilo ipasavyo.
Baadhi ya waandishi na wageni waalikwa wakifatilia jambo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: