MUGABE: HAKUNA MTU ANAYESTAHIKI NAFASI YANGU KATIKA UCHAGUZI WA 2018

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alinukuliwa jana Jumapili akisema kuwa chama chake cha Zanu-pf na wananchi hawaoni kama kuna mtu anayefaa kuchukua nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka kesho.
Rais Mugabe amesema kuwa wananchi wa Zimbabwe wanamtaka agombee uchaguzi mkuu mwakani na kwamba wananchi waliowengi wanahisi kuwa hakuna shakhsia ambaye anafaa kumrithi. Mugabe ameyasema hayo katika kukaribia kutimiza mwaka wa 93 wa umri wake wiki hii. Mugabe amekuwa madarakani huko Zimbabwe tangu mwaka 1980; na mwezi Disemba mwaka jana chama tawala Zanu-pf kilimuidhinisha kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais unaotazamiwa kufanyika katikati ya mwaka 2018 ambapo atakuwa na umri wa miaka 94.
Wakati huo huo kiongozi wa harakati ya malalamiko ya wananchi nchini Zimbabwe ametangaza kuwa atagombea kiti cha rais dhidi ya Rais Robert Mugabe katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwakani.
Mchungaji Evan Mawarire ametangaza kuchuana na Mugabe mwakani
Mchungaji Evan Mawarire aliyasema hayo nje ya mahakama mjini Harare ambapo kesi dhidi yake inatazamiwa kusikilizwa mwezi ujao wa Machi. Mwanaharakati huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na kuhatarisha usalama wa taifa, kwa kuandaa maandamano bila kibali cha serikali.

0 comments: