AMNESTY YAKOSOA UKIUKWAJI HAKI ZA BINADAMU AFRIKA MASHARIKI

Shirika la kutetea haki za binadmau la Amnesty International limekosoa ukiukwaji wa haki za binadmau barani Afrika.
Kwa mujibu wa Bi. Muthoni Wanyeki mkurugenzi wa Amnesty International katika masuala ya  Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu, mbali na kuwa kuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo hayo, pia nchi hizo zinakumbwa na hitilafu na misuguano ya ndani ya nchi.  Wanyeki amesema mazingira ya kisiasa na kijamii katika nchi kama vile Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya si ya kuridhisha. Aidha amekosoa kamatakamata ya wapinzani katika nchi kama vile Sudan Kusiini na Tanzania na kusema huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Afisa huyo wa Amnesty ameongeza kuwa kuendelea machafuko ya ndani ya nchi baina ya makundi mbali mbali kumepelekea kuibuka idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na nje ya nchi. Amesema Somalia hivi sasa ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na nje ya nchi.
Polisi nchini Kenya wakiwafyatulia waandamanaji gesi ya kutoa machozi
Wanyeki pia amebainisha masikitiko yake kutokana na kuendelea mapigano Sudan Kusini na kuelezea matumaini yake kuwa, kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo katika siku za usoni kutapelekea kuboreka hali ya mambo katika nchi hiyo changa zaidi duniani.

0 comments: