HOTUBA YA MWISHO YA MICHELLE OBAMAKATIKA IKULU YA WHITE HOUSE

Picha ya Fred MatujaPicha ya Fred Matuja
Katika siku za mwisho wa utawala wa Barack Obama, “First Lady” Michelle Obama ametoa hutuba yake ya mwisho rasmi kama mke wa Rais wa 44 Marekani. Michelle ametoa hotuba ya kuashiria mwisho wa miaka 8 ya utumishi huku akibubujikwa na machozi. Hutuba hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kuagana na mashabiki wake.
“Msiogope” Michelle Obama ameliambia kundi la walimu wa shule siku ya jumamosi, akijiandaa kuondoka katika ikulu ya White House kabla ya kuingia utawala wa Rais Donald Trump ifikapo ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu.
Tukio hilo lilikuwa jambo la tuzo kwa mwalimu mshauri wa shule 2017, isipokuwa likabadilika na kuwa kwaheri yenye hisia za mguso mkubwa.
Michelle amesema imekuwa ni “heshima kubwa sana” katika maisha yake kuwa “First Lady”, na imechukua mambo kadhaa ya kufunika kuhusiana na Bwana Trump kwa kusema ilikuwa ni jambo la tofauti na mchanganyiko wa kiutamaduni kuifanya Marekani kuwa Taifa kuu.
Machozi yalikuwa yakimtiririka kutoka machoni alipokuwa akitoa hotuba ya dakika 15 akirejea miaka 8 iliyopita akiwatumikia Wamarekani.
“Ninapomaliza muda wangu katika ikulu ya White House, ninafikiria hakuna ujumbe bora wa ku-utuma kwa vijana wetu, kwa kutoa ushauri wangu nikiwa First Lady, kwa vijana wote walio katika chumba hicho na wale wanaotazama kupitia vyombo vya habari, “mjue kuwa nchi hii ni ya kwenu”amesema kwa sauti ya mtu anaetemeka kama anaetaka kulia.
Rais Barack Obama atatoa hutuba yake ya mwisho rasmi ya kuaga jumatano ya tarehe 10 katika mji wa Chicago huko Marekani.
Binafsi nimefanikiwa kuisikiza hotuba ya Michelle Obama, imekuwa ni hotuba yenye mguso na mchanganyiko wa hisia za kuhuzunisha na furaha kwa kundi la walimu hasa wa kike waliokuwa wakimsikiza.
Nimevutiwa na maneno ya msingi aliyoyasema kwa Wamarekani; amewataka wawe na tunamini na kujipa moyo na ujasiri kwa kutoa mchango kwa maendeleo ya Marekani.
Michelle anatupa somo Watanzania kama tukiamua kujifunza kwake. Tuna wajibu wa kuishi kwa matumaini na kutumia ufahamu, maarifa na ujuzi tulio nao kuijenga Tanzania. Nchi hii ni ya kwetu. Itajengwa na kila Mtanzania mzalendo na mwenye matumaini ya kuchukua hatua ya kutoa mchango wake ili Tanzania isonge mbele.
Mfalme Daudi aliwahi kusema “Tufundishe kuhesabu siku zetu, ili tuwe na nafsi zenye hekima”.
Kila mwaka kila mtu ana siku 365 za kufanya kazi kujenga maisha yake kiufahamu, kiuchumi na kuwa na mchango chanya katika jamii inayomzunguka. Ni wakati wa kujikita katika malengo yenye kusudi la kutusogeza mbele. Manung’uniko na kulalamika
hakutabadili hali zetu kiuchumi. Bali tumaini na kupiga moyo konde kwa kutumia maarifa, ujuzi, ufahamu na kuzungukwa na watu sahihi kutakofanya kila mmoja apige hatua kimaendeleo.
Miaka 8 ya Obama imepita kama kufumba na kufumbua. Ni juzi hapa alikuwa akichuana na Senata John McCain na kumshinda. Dunia ilizizima kwa furaha na machozi. Kenya majirani zetu walitangaza siku ya mapumzuko kusheherekea ushindi wa motto ambae baba yake analizaliwa Kenya.
Tuna wajibu wa kupigania kile tunachokiamini ambacho kinajenga misingi yetu ya kukua ili siku moja tumeaga dunia, watoto wetu na wajukuu zetu wana jambo la kijivunia kufuatia alama yenye mguso katika jamii ambayo tumeiacha.
Kwa uzoefu wangu wa kusoma vitabu vya mashujaa, sikuwahi kuona shujaa anaebadilisha maisha yake na watu wake kwa kuamini habari hasi za kukatisha tama. Shujaa ni yule alieamua kubadili maisha magumu kwa juhudi na maarifa ili kuondoa ule ugumu kwa kushirikana na watu wenye nia chanya yenye kuamini kuwa inawezekana.
Tanzania itajengwa na mtu mmoja na makundi ya watu wenye mtazamo wa matumaini ya kutatua matatizo ili siku za usoni ziwe bora kuliko leo. Kukiwa na mtazamo chanya na kuchukua, hatua za makusudi, Tanzania ya kesho itakuwa mahali bora pa kuishi.
Mungu Ibariki Tanzania. Kwa pamoja tunalijenga Taifa letu.
Fredrick Matuja

0 comments: