MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAUGUZI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA WA PILI WA CHAMA CHA AKIBA NA KUKOPA

 Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tanzania cha Akiba na Kukopa (SACCOS), Adam Leyna (wa tatu kushoto)  akifungua Mkutano Mkuu wa pili wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Makuti wa JKT Mgulani Dar es Salaam.  Kutoka kushoto ni, Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Scholastica Maganga, Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Rosemary Mkosamali na wa kwanza  kulia ni Meneja wa Ngome Saccos, Sudi Mangara
 Mshehereheshaji akiendesha Mkutano huo, ambaye ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Clauda Mlombo
 Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Shaibu Ally akiongoza ufunguzi wa Sala katika Mkutano huo
 Viomgozi wakiwa meza kuu, kunzia kulia ni, Meja, Lea Mtuma akimwakilisha Mkuu wa Jeshi la kujenga Tafa (JKT ), Meneja wa Ngome Saccos, Sudi Mangara,  Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tanzania cha Akiba na Kukopa (SACCOS), Adam Leyna, Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Rosemary Mkosamali na Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Scholastica Maganga
 Afisa Muuguzi Mkuu Hospitali ya Lugalo, Devota Mutayoba akiongoza ibada katika mkutano huo 
 Muuguzi akifatilia jambo kwa umakini mkubwa


 Wauguzi  wakiimba wimbo wa chama chaokatika mkutano huo

 Na Khamisi Mussa

 MWENYEKITI wa Chama Cha Wauguzi Tanzania cha Akiba na Kukopa (SACCOS), Adam Leyna amewaomba wanachama ambao ni wauguzi kuchangamkia fursa ya mikopo kutoka katika chama hicho  na kuachana na kukimbilia kukopa katika mabenki ambayo yanatoza riba kubwa.

Leyna aliyasema hayo wakati jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu huo ambapo alitoa wito kwa wauguzi wote nchini kujiunga na Saccos hiyo kwani ni mali yao.

"Saccos hii ni yetu na ipo kwa sababu maalumu ya kiinua uchumi wa wanachama ili tujikomboa na changamoto ya maisha tuliyonayo" alisema Leyna.

 Leyna aliwataka wauguzi hao kuhamasishana ili kupata wanachama wengi ili kukuza chama hicho ambacho ni muhimu kwao.

 Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Rosemary Mkosamali (kulia) akimkabidhi kadi ya uanachama,  Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Kirwa Mashati kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, Theopista Njau
 Wanachama wakiserebuka
 Wanachama wakiserebuka
 Wanachama wakiserebuka
 Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni,  Rosemary Mkosamali (kulia) akimkabidhi kadi ya uanachama Afisa Mfawidhi Daraja la Kwanza Hospitali ya Taifa Muhimbili, Violet  Minja

Picha ya pamoja . (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

0 comments: