VUMBI NA MOSHI WA SUMU UMESABABISHA VIFO VYA WATU LAKI MOJA INDONESIA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:13 PM
Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanywa
yameonyesha kuwa kuna uwezekano kwamba vumbi la moshi wa sumu uliotokana
na moto uliowashwa mwaka uliopita katika maeneo ya misitu ya Indonesia
vimesababisha vifo vya kabla ya wakati vya watu wapatao laki moja katika
maeneo hayo.
Matokeo ya uchunguzi huo uliofanywa na watafiti wa vyuo vikuu
vya Harvard na Columbia nchini Marekani unaonyesha kuwa kuna uwezekano
mkubwa sana kuwa "vumbi na moshi thakili" ambao ulitanda katika maeneo
hayo ya Indonesia kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba mwaka uliopita wa 2015
ndio uliosababisha vifo vya kabla ya wakati vya watu zaidi la elfu
tisini.
Matokeo ya uchunguzi huo yaliyochapishwa leo katika jarida la
intaneti la "Barua za Utafiti wa Mazingira" aidha yamekadiria kuwa vumbi
hilo la moshi huenda ndilo lililosababisha pia vifo vya watu wengine
elfu moja katika nchi jirani na Indonesia za Singapore na Malaysia.
Hii ni katika hali ambayo serikali ya Indonesia ilikuwa imetangaza
hapo awali kuwa ni watu elfu 19 tu ndio waliofariki dunia kutokana na
athari ya vumbi na moshi huo wa sumu.
Vumbi na moshi uliotokana na moto uliowashwa mwaka uliopita katika
maeneo ya misitu nchini Indonesia uliendelea kutanda katika maeneo hayo
kwa muda wa wiki kadhaa.
Moto huo uliwashwa kwa lengo la kupatikana maeneo zaidi ya ardhi kwa
ajili ya kilimo cha michikichi ya uzalishaji mafuta ya mawese.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: