KIONGOZI MUADHAMU WA MAPINDUZI YA KIISLAMU AUPONGEZA MSAFARA WA MICHEZO YA PARALIMPIKI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:08 PM
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
ametoa ujumbe kwa msafara wa michezo ya Paralimpiki wa "Mashahidi wa
Mina" na kueleza kwamba:"Mliyofanya ni ya kujivunia na mumelifurahisha
taifa la Iran".
Katika ujumbe huo wa Ayatullah Khamenei kwa wanamichezo wa Iran
katika mashindano ya wanamichezo walemavu ya Paralimpiki ya Rio
imeelezwa kuwa:"Mumelitangaza jina lenye heshima la mashahidi madhulumu
wa Mina katika anga ya dunia na kulionesha vazi lililobarikiwa la Ihramu
mbele ya maadui wa nembo za Kiislamu".
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa shukrani kwa
msafara wa michezo ya Paralimpiki wa Mashahidi wa Mina na kuongeza kuwa
ana matumaini kwamba kwa kushikamana na misingi ya sharia za
dini wanamichezo wa Iran, kama ilivyo kila mara, watashiriki katika
medani za michezo wakiwa na moyo wa kujiamini ambayo ni sifa
wanayostahiki kuwa nayo wanamichezo wa Kiirani.
Ayatullah Khamenei vilevile ametoa mkono wa pole kwa msiba wa kuhuzunisha wa mwanamichezo majeruhi wa vita Bahman Golbadnejad.
Msafara wa Paralimpiki wa Iran katika michezo ya Rio 2016
umekamilisha mashindano hayo kwa kushika nafasi ya 15 baada ya
kujinyakulia medai 8 za dhahabu, 9 za fedha na 7 za shaba.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: