SIKIO SIKIVU LAHITAJIKA KULETA MAPINDUZI YA ELIMU DUNIANI- KIKWETE

Mmoja wa kamishna rais mstaafu Jakaya Kikwete.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/video capture).
Mmoja wa makamishna wa tume ya kimataifa ya kusaka uchangishaji kwa elimu Duniani, amesema mapendekezo yao ya kuinua kiwango cha elimu yasipozingatiwa, watoto wengi zaidi hatawakuwepo shuleni ifikapo mwaka 2030.
Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania ameiambia Idhaa hii jijini New York, Marekani baada ya uzinduzi wa ripoti yao kuwa, Mapendekezo yao ni pamoja na mbinu mpya za uchangishaji ikiwemo taasisi za kimataifa za kibenki akisema kinachohitajika..
Ripoti hiyo inasema serikali zisipowezeka katika elimu, watoto katika nchi hususan za kipato cha chini watatwama kwenye mzungumzo wa umaskini na kusalia bila stadi zinazohitajika. (P.T)

0 comments: