WANAFUNZI 200 WANAOTARAJIA KUONDOKA LEO KUSOMA VYUO VYA NJE WAPIGWA MSASA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:20 PM
Mkurugenzi
Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza
katika semina ya wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka leo
kwenda vyuo vikuu vya nchini China, iliyofanyika katika ukumbi wa
Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wanaokwenda nje wakichukua
tiketi pamoja na viza kwa ajili ya safari kwenda katika vyuo vikuu vya
nchini China iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya
wazazi na wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Globa
Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel hayupo pichani katika semina
iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel amesema
wanafunzi wanaokwenda nje waliohitimu masomo katika vyuo vya nje
wanatakiwa watafutwe na waajiri na sio wawe wa kutafuta ajira.
Mollel
ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa semina na wazazi na
wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka leo katika vyuo vikuu vya nchini
China, amesema kuwa kutokana na vyuo hivyo kuwa na vifaa vya kujifunzia
wanafunzi wakitumia vizuri katika soko la ajira watatafutwa.
Mollel
amesema nchi haina tatizo la ajira hivyo watu wanatakiwa kuwa na uwezo
binafsi ambao utamfanya mwajiri kutafuta mtu wa kumuajiri hivyo
wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo wanatakiwa kutumia maarifa ya kuja
kuzalisha nchini.
Amesema
wazazi watumie muda wao katika kuwafuatilia watoto wao wanaosoma nje ili
kuweza kuona thamani ya fedha wanazozitoa na elimu wanayoipata.
Aidha
amesema kuwa wale ambao wanahitaji vyuo vya nje bado nafasi zipo na
wanafunzi wote watafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja Tume ya Vyuo
Vikuu nchini kujiridhisha na vyuo wanavyokwenda. Mollel amesema
haitakuwa tayari kuona wanafunzi wanahitimu vyuo vya nje kupitia GEL
kuwa hawatambuliki. (P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: