DUDUMIZI KUZINDUA APPLICATION INAYOWEZESHA WAFANYABIASHARA KUUZA NA KUWAFIKIA WATEJA KIURAHISI POPOTE WALIPO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:54 PM
Tunayofuraha kuwataarifu wana Dudumizi na jamii kwa
ujumla kuwa, baada ya kukaa jikoni kwa muda mrefu, tunatarajia kuzindua
programu yetu ya mauzo, inayojulikana kama Michongo App. Application
hii ya Michongo inakuwezesha kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zilizopo
kwenye punguzo.
Michongo inajitofautisha na programu nyingi za mauzo ya online kwa sababu kuu zifuatao;
1. Michongo inauza bidhaakwa bei ambayo hauwezi kuipata sokoni. Inamaana, Michongo imeshabageni bei kwa ajili yako.
2. Michongo inatumia programu rafiki ya Affiliate kuwezesha watu
kuingiza kipato kwa kila linki wanayosambaza kwa marafiki zao na rafiki
akanunua bidhaa. Hii inamaanisha, Michongo ni agent wa timu ya sales
itakayokufanyia kazi. Kwa mtindo huu, unaweza kupunguza gharama za
kutangaza biashara yako hadi nusu kwa sababu hakuna gharama yoyote kwa
kutangaza kwenye Michongo, pia kuna mamilioni ya watu watakuwa busy
kusambaza link za bidhaa yako. Hii itawawezesha wajasiriamali wadogo
wengi kuingia sokoni na kutengeneza ajira zaidi na zaidi, kama malengo
ya Rais wetu (kuongeza ajira).
3. Michongo inakuwezesha kupata huduma kwa kutumia namba za kuponi.
Hii inamaana, unaepuka kutembea na pesa (usalama) na malipo yote
yanaishia kwenye Michongo na kukupa namba ya siri utakayoonesha kwa
muuzaji.
4. Michongo inahusisha Bidhaa na Huduma. Programu nyingi zimejikita
kwenye bidhaa pekee huku zikisahau Huduma. Michongo tumekufikia.
5. Michongo inakuwezesha kupata bidhaa zilizo karibu nawe zaidi kwa
kutumia simu ya mkononi. Chukulia upo katikati ya mji na unataka
kutafuta sehemu yenye punguzo la chakula ukapate chakula cha mchana.
Utapata kwenye Michongo App.
Katika uzinduzi huu, Michongo inaandaa tamasha la mauzo ambapo
wafanya biashara watapata kuuza moja kwa moja bizaa na wateja kununua.
Tamasha hili linaitwa Michongo festival .
Michongo festival ni tamasha la aina yake kuwahi kutokea Tanzania
ambapo wauzaji wataweza kuuza moja kwa moja, pia watapata nafasi ya
kujua zaidi kuhusu michongo, kwakweli si la kukosa. Tamsaha hili
litafanyika Oktoba 29, Mlimani City
Idea hii ya Michongo ilianzia nchini China ambapo muanzilishi wa
Dudumizi Mr Nyoni aliliwasilisha wazo la Michongo kwenye kongamano
la wana electronics Duniani lililohudhuriwa na magwiji kutoka kampuni
makubwa ya teknolojia Duniani, kama Intel, IBM, Microsoft na mengine
mengi. Katika kongamano hilo Mr Nyoni alialikwa kama mtoa mada mkuu (Keynote Speaker)
ambapo aliweza kuliwasilisha wazo la Michongo na jinsi gani litasaidia
kukuza biashara kwa nchi zinazoendelea haswaa kwenye dunia ya leo ya
mitandao, baada ya miaka mitano, leo hii anatimiza wazo hili.
Wazo kamili la Michongo ni
kuweza kufikisha huduma au bidhaa kwa uharaka, kwa watu wengi na bei
nafuu, huku ukimsogezea mnunuzi bidhaa karibu na pia zilizo na machaguo
yake. Mnunuzi anapata bidhaa zilizomlenga na zinazomfaa (selected) na zilizomzunguka (nearby)
huku tukiongeza ushinani kwa watoa huduma. Michongo inalenga kuwapa
sauti wanunuzi na kuwapa nafasi ya kuwashawishi wengine zaidi kununua
bidhaa/huduma.
Kujua mengi zaidi kuhusu Michongo na Michongo Festival tembelea http://festival.michongo.co.tz/ na kushiriki kwenye Michongo festival jisajili online kwa kwenda http://festival.michongo.co.tz/register-business.html
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: