ROONEY AMWAGA MACHOZI, ATOA UJUMBE MZITO KWA WENZAKE

Rooney 54Baada ya kuvunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya England kwa kufikisha magoli 50 hivi sasa, Wayne Rooney alijikuta mwenye hisia kubwa mbele ya wachezaji wenzake na mashabiki waliokuwa wakimpongeza mara baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 84.Rooney mwenye miaka 29 alitokwa na machozi huku akinyoosha mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu kwa mafanikio aliyoyapata katika maisha yake ya soka.

Akiongea katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kuombwa kufanya hivyo na kocha Roy Hodgson, Wayne amesema ni wakati mkubwa na muhimu kwake na familia yake huku akiwapa changamoto vijana Raheem Sterling, Harry Kane na Ross Barkley kukomaa na kufikia hadi kupita rekodi yake siku zijazo.
Rooney 53Wachezaji lukuki wakiongozwa na David Beckham wamempongeza mchezaji huyo huku nahodha wa Chelsea, John Terry akienda mbali zaidi kwa kusema Rooney ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kuzaliwa England.
Chama cha soka England, FA kitamfanyia sherehe nahodha huyo wa England mwezi ujao katika mechi ya kufuzu itayofanyika Wembley katika usiku utakaoitwa Wayne Rooney ambapo atakabidhiwa kiatu cha dhahabu na Sir Bob Charlton ambaye ndiye alikua akishikilia rekodi hiyo kwa miaka 45 sasa.

0 comments: