NDEGE YA BRITISH AIRWAYS YAUNGUA

1
Ndege ya British Airways ikiungua katika Uwanja wa Ndege wa McCarran uliopo Las Vegas.
2
Ndege ya British Airways aina ya Boeing 777  baada ya kuzimwa moto huo.

3
Abiria wakishuka katika ndege hiyo baada ya moto kuzimwa.
4
Ndege hiyo baada ya kuzimwa moto.
56
Picha iliyopigwa na abiria aliyekuwa kwenye ndege nyingine.
7
NDEGE ya British Airways iliyokuwa na watu 172 imeungua wakati ikijiandaa kupaa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran uliopo Las Vegas nchini Marekani jana usiku.
Katika ajali hiyo, watu 14 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu ila hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa inajiaanda kupaa kuelekea jijini London wakati ilipoanza kuwaka moto baada ya kupata hitilafu katika mfumo wake wa injini.
Vikosi vya zimamoto katika Uwanja wa McCarran vilifanya kazi ya ziada kuzima moto huo kabla ya kuleta madhara makubwa.
Majeruhi katika ajali hiyo wengi walipata madhara kutokana na moshi mkubwa uliokuwa ukitoka katika ndege hiyo.
Kati ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo, 159 walikuwa abiria huku 13 wakiwa wafanyakazi wa ndege hiyo.
Credit: Daily Mail

0 comments: