MWENYEKITI WA CCM DR.JAKAYA KIKWETE AMNADI DR. JOHN POMBE MAGUFULI MOROGORO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 3:41 PM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano wa kumnadi mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Morogoro mkoani
humo ambapo maelfu ya wananchi mjini Morogoro wamehudhuria katika
mkutano huo.
Dr. John Pombe Magufuli
amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka
huu na kumchagua ili aweze kuwatumikia watanzania kwa ujumla wake na
kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo ya watanzania ili
kuipaisha Tanzania katika maendeleo.
Ameongeza kwamba yeye atakuwa
rais wa watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama, Makabila, Dini
wala Ukanda kwani maendeleo hayana vyama, Kabila, Dini wala Ukanda ila
ni kwa watanzania wote.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye
uwanja wa jamhuri kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku
wakiwa wameshika kofia zao.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakifuatilia jambo huku wakiwa na sura
za tabasam wakati Mzee Yusuf Makamba akihutubia wananchi mkoani Morogoro
kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Bw. Innocent Kalogeres.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
mkoani Morogoro na kuomba kura kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja
wa Jamhuri mkoani humo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akisistiza jambo katika mkutano huo.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John
Pombe Magufuli akimnadi Mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Mh.
Mohamed Abood.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya
Uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Mh. Mohamed Abood.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM Ndugu Abdallah Bulembo akiwahutubia wananchi wa Morogoro katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mzee Yusuf Makamba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakiimba wimbo katika mkutano huo kulia
ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Morogoro Bw. Innocent Kalogeres.
Mzee Yusuf Makamba akiwahutubia wananchi wa Morogoro katika mkutano huo.
Msanii Ali Kiba akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano huo.
Kundi la Wasanii wa Filamu nchini la Mama Ongea na Mwanao likitumbuiza katika mkutano huo.
Kundi la muziki la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akipunga mikono kwa
wananchi waliofurika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati
akiwasili uwanjani hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Mzumbe wakimpokea Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. John Pombe Magufuli wakati akielekea mjini Morogoro.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi
akiwa njiani kutoka Ifakara kwenda Kilosa mkoani humo.
Baadhi ya watoto wakiwa
wameshikilia picha ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kilosa.
Baadhi ya Watawa wakifurahia
jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John
Pombe Magufuli akizungumza mjini Mikumi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa
jimbo la Mlimba Bw.Godwin Emmanuel Kunambi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombeaJonas Estomih Nkya.
Mmoja wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo akifurahia jambo.
Wananchi wa Kilombera wakinyanyua mabango yao juu juu wakati wa mkutano huo.
“Hapa ni Kazi tu”
Steven Nyerere anakamua tu hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: