MUFTI MKUU WA TANZANIA WA TANZANIA BAADA YA MUFTI SIMBA KUFARIKI DUNIA JULAI MWAKA 2015

Mkutano mkuu wa baraza kuu la waislamu Tanzania Bakwata umempitisha Sheikh Abubakary Zubeir kuwa mufti mkuu wa awamu ya tatu wa Tanzania baada ya kukosa mpinzani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huku akiwataka waumini wa dini hiyo kuliombea taifa amani katika kipindi hiki cha kampeni mpaka kufanyika kwa uchaguzi mkuu na kutangazwa kwa matokeo yake.


Sheikh Abubakary Zubeiry amechaguliwa kuwa mufti wa Tanzania baada ya mpinzani wake Sheikh Ali Mkoyogole kujitoa dakika za mwisho kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kwa madai kuwa anaridhika na utendaji wa Sheikh Zubeir ambaye awali alikuwa kaimu mufti kufuatia kufariki kwa aliyekuwa mufti mkuu wa tanzania wa awamu ya pili Sheikh Shaaban Issa Bin Simba Jully mwaka huu.
Muda mfupi baada ya uteuzi huyo mufti Zubeiry alipata fursa ya kuzungumza na wajumbe wa Bakwata ambapo pamoja na mambo mengine amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuliombea taifa amani wakati linakabiliwa na changamoto ya uchaguzi mkuu ujao huku akitoa wito kwa watanzania kushiriki mchakato huo kwa utulivu ili kuilinda tunu ya amani na upendo ambayo tanzania imekuwa ikijivunia kwa muda mrefu.
Akitoa salamu katika baraza hilo mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa wamewataka viongozi wa dini ya kiislamu kuendelea kuhubiri na kufundisha waumini mafunzo ya kiroho ili kudumisha amani ya nchi lakini pia wasisahahu kusisitiza elimu dunia ili taifa na watu wake kuondokana na utegemezi.


Kwa upande wao baadhi ya Masheikh ambao ni wajumbe wa baraza kuu la bakwata wametoa maoni yao kuhusu mufti huyo huku pia wakizungumzia nafasi ya waislamu katika uchaguzi mkuu ujao.
Uchaguzi wa mufti mkuu wa Tanzania awali ulikuwa na wagombea wanne ambao ni mufti aliyechaguliwa na aliyejitoa pamoja na masheikh wengine wawili ambao waliyeenguliwa katika kinyang’anyiro hicho na baraza la maulamaa nchini ambao ni Sheikh Hamis Abass Mtupa na Hasan Ibrahim Kiburwa.

0 comments: