Waliojaribu kuzuia mashambulio hayo waliuuwawa. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu elfu mia moja thelathini wamefurushwa makwao kuanzia Januari mwaka huu. Wengi wao sasa wanaishi misituni.
Baadhi ya waliobakwa pia bado hawajapokea matibabu yoyote.
Human Rights Watch wakati huohuo pia imeshutumu vikali viksoi vya pamoja vya Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambavyo vinahudumu katika eneo hilo kwa kutowajibika ipasavyo kuwalinda raia. Ripoti hiyo aidha imependekeza serikali ya Sudan kuondoa vikosi hivyo katika eneo hilo mara moja na kuchunguza madai hayo.
Ripoti hiyo yenye kurasa 88 inasema matukio hayo yalitekelezwa katika eneo kubwa na kwa ukatili mkubwa. Zaidi ya mashahidi mia mbili waliohojiwa, wengine wakiwa katika mataifa ya Chad na Sudan Kusini ambako wamekimbilia hifadhi. "RSF imeuwa, kubaka na kuwatesa raia wengi katika vijiji, katika mashambulio ambayo yalipangwa awali, " alisema mkurugenzi wa HRW barani Africa Daniel Bekele,
" Serikali ya Sudan ni lazima iwapokonye silaha mara moja vikosi hivi na kuwafungulia mashtaka makamanda wote waliohusika." aliongeza
Mapigano yalizuka katika eneo la Darfur, Magharibi mwa Sudan Mwaka wa 2003, baada ya waasi waliojihami kuanza kupinga kutengwa na serikali ya Omar al Bashir. Kiongozi huyo anasakwa na Mahakama ya Kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kwa madai ya kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za kibindamu katika eneo hilo.
AS
0 comments: