MAKAMU WA RAIS AKIHUTUBIA WAKATI WA HAFLA YA KUFUNGUA KITUO CHA POLIZI DARAJA "A" WILAYA YA KIPOLISI MTUMBA NA KUKABIDHI MAGARI 21.

 





 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kufuata taratibu, kuzingatia sheria ya Jeshi la Polisi na kanuni za Polisi katika kufanya kazi   za   Kipolisi   ikiwemo   kukamata,   kufanya   upekuzi,   kushikilia, kupeleleza   watuhumiwa   pamoja   na   kuwahoji   mashahidi   na watuhumiwa.


Makamu  wa   Rais   ametoa   wito   huo   wakati   wa  ha"a   ya   kufungua Kituo cha Polisi Daraja “A” Wilaya ya Kipolisi Mtumba na Kukabidhi Magari   21   kwa   Jeshi   la   Polisi,   ha"a   iliyofanyika   eneo   la   Mtumba Mkoani   Dodoma.   Amesema  Maadili   mema,   nidhamu   kazini   na uwajibikaji ni nguzo muhimu kwa Jeshi la Polisi katika kusimamia sheria.   Makamu   wa   Rais   amelipongeza   Jeshi   la   Polisi   pamoja   na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa kuendelea kuimarisha Amani na usalama hapa nchini.


Aidha   Makamu   wa   Rais   amesisitiza   umuhimu   wa   Jeshi   la   Polisi kubadilika   kwa   haraka   ili   kuweza   kukabiliana   na   mbinu   mpya   za uhalifu kwa kuongeza kasi ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli zake. 


Amewasihi kujielekeza zaidi katika kubuni na kutumia mifumo ya   TEHAMA   na   kuhakikisha   Askari   na   Makamanda   wanapata mafunzo   ya   mara   kwa   mara   kwenye   maeneo   ya   intelijensia, usalama   na   uhalifu   wa   kimtandao,akili   mnemba   na   matumizi   ya roboti  pamoja   na   kuunganisha  Makao   Makuu   ya   Jeshi  la   Polisi   na Mikoa,   Wilaya,  Vikosi,   Vitengo  na   Vituo  vyote  vya  Polisi   nchini   ili kurahisisha mawasiliano.


Vilevile Makamu wa Rais amelitaka Jeshi la Polisi nchini  kuangalia upya mfumo mzima wa utoaji leseni, ukaguzi wa magari, matumizi ya teknolojia hususan kamera za barabarani na matumizi ya Body-cam   jackets    zitakazoonesha   mazungumzo   baina   ya   askari   na madereva   ili   kudhibiti   rushwa   barabarani,kuimarisha   weledi   na uthabiti wa vyombo vya moto hali itakayosaidia katika kudhibiti ajali za barabarani.


Halikadhalika  Makamu  wa  Rais   amesema  ni   muhimu kwa  Jeshi  la Polisi   kujenga   uhusiano   mzuri   kati   yake   na   wananchi   ili   liweze kufanikiwa   kubaini,   kuzuia   na   kudhibiti   uhalifu   wa   aina   zote.   Pia ameitaka jamii kuheshimu sheria na taratibu za Jeshi la Polisi wakati 

wa utekelezaji wa majukumu yao. Amesema Jitihada zinazofanyika kupitia dhana ya Polisi Jamii ni budi ziendelezwe.


Makamu   wa   Rais   ameitaka   Wizara   ya   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi kufanyia   kazi   mapendekezo   ya   Tume   ya   Kuangalia   Jinsi   ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai yaliyo ndani ya uwezo wake  ikiwemo kuimarisha Madawati ya Malalamiko ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya   Nchi   na   Jeshi   la   Polisi   kwa   kuyapatia   watumishi   wa   kutosha wenye   weledi   kwenye   masuala   ya   uchunguzi   ili   kuendelea kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi nchini.


Kwa   upande   wake   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi   Mhandisi Hamad   Masauni   amesema   Jeshi   la   Polisi   limeendelea   kukuza matumizi   mbalimbali   ya   mifumo   ya   TEHAMA   ikiwa   ni   utekelezaji maelekezo   ya   Mheshimiwa   Rais   katika   kuleta   ufanisi,   uwazi   na uharaka wa kazi za Kipolisi kwa lengo la kuharakisha masuala yote ya haki jinai na kuhakikisha yanatendeka kwa tija.


Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema Jeshi   la   Polisi   linatambua   deni   kubwa   walilonalo   kwa   Serikali   na Wananchi hivyo litazidisha utendaji wenye nidhamu ya hali ya juu, haki, uadilifu na kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi ni huduma sahihi na zinazotakiwa. 


Ameongeza   kwamba   ujenzi   wa   Vituo   hivyo   vya   kisasa   vya   Polisi utawezesha kutafsiri madhumuni halisi ya kuwepo kwa Jeshi la Polisi kwa kuwa majengo hayo ni ra3ki hata kwa watendaji katika kutimiza wajibu wao. (NA MAKAMU WA RAIS).

0 comments: