DKT. TULIA AKUTANA NA VIONGOZI WAKUU GENEVA

 


   Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi Spika wa Algeria Mhe. IBrahim Boughali, zawadi ya ngao yenye kuakisi IPU na asili ya Tanzania katika Ofisi za Makao Makuu ya IPU, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 17 Mei, 2024 wakati wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 6 Maspika wa Mabunge Duniani unaotarajiwa kufanyika mwakani.
   Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Spika wa Qatari Mhe. Hamda Bint Hassan Al-Sulaiti, katika Ofisi za Makao Makuu ya IPU, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 17 Mei, 2024 wakati wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 6 Maspika wa Mabunge Duniani unaotarajiwa kufanyika mwakani.
   Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiwa katika mazungumzo leo tarehe 17 Mei, 2024 wakati wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 6 Maspika wa Mabunge Duniani unaotarajiwa kufanyika mwakani.

PICHA NA OFISI YA BUNGE

0 comments: