Mwamko mdogo wa Watanzania kuhusu bima ya afya ni mojawapo ya changamoto katika kutoa huduma bora za afya kwa wote kutokana na idadi ndogo ya Watanzania wenye bima. Takwimu za Wizara ya Afya (2022) zinaonesha kuwa asilimia 15 tu ya Watanzania, sawa na watu milioni 9.1, walikuwa na bima ya afya mwishoni mwa mwaka 2021, ikishuka kutoka asilimia 32% mwaka 2018.
Vodacom Tanzania PLC imeungana na Assemble Insurance na kuja na bima ya afya ya kijiditali kupitia simu ya mkononi iitwayo AfyaPass ambayo ni rahisi, nafuu, na inapatikana kwa Mtanzania popote pale alipo nchini. Bima hii inapatikana kwa bei nafuu ya Shilingi 70,000 kwa mwaka kwa mtu mmoja na vifurushi vya familia kutoka TZS 105,000 kwa watu wawili hadi TZS 385,000 kwa watu sita kwa mwaka na inapokelewa katika hospitali binafsi na za serikali. Kwa malipo kidogo ya nyongeza, mtumiaji anaweza kupata huduma za uzazi, radiolojia, mazoezi tib ana nyingine nyingi.
Unaweza kujiunga na AfyaPass kupitia M-Pesa ikiwa ni moja ya aina za bima zinazotolewa kupitia VodaBima yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima kwa kila mtu bila kujali kipato chake au umbali wa eneo anapotoka nchini Tanzania.
0 comments: