LIBYA INAHITAJI MSAADA WA KIBINADAMU WA DOLA MILIONI 313
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:19 PM
Mapigano yangali yanaendelea nchini Libya
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa
Mataifa nchini Libya, amezindua mkakati wa kushughulikia maafa ya
kibinadamu mwaka huu wa 2018 nchini Libya.
Mpango
huo uliozinduliwa na Bi Maria do Valle Ribeiro unalenga kuchangisha
dola millioni 313 za kutumiwa kwa ajili ya msaada wa kuokoa maisha ya
watu karibu milioni moja.
Mpango
mkakati huo (HRP) umezinduliwa kwa niaba ya jumuiya ya wahisani wa
misaada ya kibinadamu kwa ushirikiano na wakuu wa mamlaka ya Libya.
Ombi
hili ni la tatu kutolewa na litasaidia kutekeleza miradi 71,
inayoendeshwa na asasi za kiraia 22 mkiwemo mashirika ya Umoja wa
Mataifa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi, Riberio, amesema wananchi wa Libya hupitia matatizo
makubwa, kupata mahitaji muhimu na kuongeza kuwa ni sharti wawe chonjo
dhidi ya athari za kutofanya jambo lolote kuhusu hali hiyo.
Miradi hii ina nia ya kutoa ulinzi kwa raia wa kawaida, kulingana na
sheria za kimataifa, ili kuhakikisha kuwa watu wanapata huduma bora
mfano wakimbizi wa ndani, watu wanaorejea kutoka ukimbizi au uhamishoni
pamoja na raia walioko Libya ambao hawakupoteza makazi yao kama vile
wahamiaji, wakimbizi na watafuta hifadhi.
Fedha
hizo pia zitasaidia familia kupata uwezo wa kukidhi maisha yao dhidi ya
shinikizo zinazoendelea za kuporomoka kwa uchumi, mparaganyiko wa
familia pamoja na hali ya kukosekana kwa amani.
Libya
ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa na hali ya mchafukoge tangu
kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kufuatia
uingiliaji kijeshi wa Marekani na waitifaki wake katika Muungano wa
Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato). Kwa sasa Libya ina serikali mbili
hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk na nyingine ya ni ya Umoja
wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na ina makao yake mjini
Tripoli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: