ASKARI 7, NA RAIA 1 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIZI YA MABOMU SOMALIA

Kwa akali askari saba wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yalilolenga msafara wa magari ya majeshi karibu na mji wa Baidoa nchini Somalia.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limetangaza kuhusika na hujuma hizo na kudai kuwa, limeua askari kadhaa wa Somalia na wengine wa Ethiopia wanaohudumu chini ya mwavuli wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM.
Duru za polisi zimearifu kuwa, shambulizi la kwanza lililenga msafara magari ya jeshi uliokuwa ukitoka katika wilaya ya Wajid, jimbo la Bakol kuelekea Baidoa abapo wanajeshi wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Wanachama wa al-Shabaab nchini Somalia
Katika shambulizi la pili, msafara wa magari ya jeshi uliripuliwa na mabomu ya kutegwa ardhini katika eneo la Goofgaduud, yapata kilomita 35 kaskazini mwa mji wa Baidoa, kusini magharibi mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika na kuua askari watatu.
Huku hayo yakiarifiwa, mtu mmoja aliuawa hapo jana na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi la bomu la kutegwa garini, katika mji mkuu Mogadishu.
Wanajeshi wa AMISOM
Mohamed Hussein, afisa mwandamizi wa polisi mjini humo amethibitisha kutokea hujuma hiyo na kufafanua kuwa, mwanamke mmoja aliuawa na mwanamme alijeruhiwa baada ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali mjini Mogadishu kuripuka. 

0 comments: