CHADEMA YAISHAURI SERIKALI KUHUSU MCHANGA WA MADINI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeishauri serikali kujenga kinu cha kusafishia mchanga wa dhahabu hapa nchini, huku ikifanya marekebisho ya sheria ya madini, ili kuondoa mianya ya ukwepaji wa kodi katika madini.

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la (CHADEMA) mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema hakuna sababu za msingi za kutojengwa kwa kinu hicho hapa nchini.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa (CHADEMA) akatoa suluhu, juu ya hatua ambazo serikali inatakiwa kuzichukua, badala ya kuingia mgogoro na wawekezaji.


Pamoja na mambo mengine, chama hicho cha upinzani nchini, kimetoa msimamo wake kuwa sasa kina muunga mkono mgombea wa Jubilee katika uchaguzi mkuu Kenya, ambaye ni Rais wa sasa, Uhuru Kenyata, huku wakitoa sababu ni kwanini wameamua kumuunga mkono mgombea huyo.

0 comments: