WAGENI VIJANA WEKEZENI KWENYE HISA KIGOMA NA RC RUYUGI ATOA NENO KWA WARUNDI BUJUMBULA


Na Magreth Magosso,Bujumbula
MKUU wa Mkoa wa Ruyigi Nchini Burundi Abdallah Hassan, amewataka warundi wote walioko nje ya Nchi hiyo kwa madai ya Ukimbizi ,warudi nchini humo,ili kuinua uchumi,umoja na mshikamano wenye manufaa ya kulijenga taifa hilo.

Akitoa kauli hiyo hivi karibuni mkoani ruyugi baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kuzulu mkoani hapo kama sehemu ya kuimarisha ujirani mwema baina yao,huku akisisitiza  raia wa burundi waliokimbia machafuko, kwa sasa hawana sababu ya kufanya hivyo, kutokana na hali ya usalama na utulivu kuimarika kila kukicha na kuwataka warudi  ili, kuinua uchumi wao kwa ujumla.

Hassan aliongeza kuwa baada ya machafuko ya kisiasa ya mwaka 2015, raia wao bado wanakimbia kwa madai ya machafuko ambayo hivi sasa hayapo na kuwataka kurejea na kuipenda nchi yao kwa kuwa burundi itajengwa na kulindwa na warundi wenyewe na si watu wengine .

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kibondo  Tanzania Luis Bura , aliishauri  Serikali ya Burundi kutengeneza mazingira salama yenye kuhamasisha na kuwarudisha watu wake nchini mwao, kwa kuwa amani ipo na kuonya warundi wanaokimbia na kuingia kigoma kupitia kambi za wilaya ya kibondo kuwa,hawana sifa za ukimbiazi.

“katika kujiridhisha na utulivgu uliopo hapa,kamati ya ulinzi ya wilayani kibondo tumezuia   kupokea wakimbizi wasiokidhi sifa ya ukimbizi na kambi za kibondo hatupokei ,lakini wekeni mazingira rafiki watu wenu warejee kwa amani” alisisitiza Bura.

Na Jiji la Bujumbula linalodaiwa kukubwa na machafuko  mwaka 2015,lakini kwa sasa hali shwari wakazi wake wakiendelea na shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambapo Majira ilibahatika kufanya mahojiano na Buchumi Shomari na Ngenda Banka kwa nyakati tofauti waliwatoa hofu ndugu,jamaa na rafiki zao waliokimbia warudi kwa kuwa kuna usalama wa kutosha.
 Wakati huohuo wakazi wa mkoa wa Ruyigi ambao wanaishi karibu na Nchi ya  Tanzania, Hamida Kharufan na Didas Luzovil kwa nyakati tofauti walifafanua kuwa,kilichobaki kwa sasa warundi wengi wanakimbia njaa na kutoa wito kwa wenzao warudi Burundi wakafanye kazi kwa maslai mapana ya taifa lao

“Sisi hivi sasa nchi nzima ya Burundi tunasafiri usiku kilometa nyingi bila kubugudhiwa na Mtu yeyote kutokana na utulivu uliopo sasa, hao wanaoendelea kuitoroka nchi  wanakimbia nini  warudi tujenge nchi yetu,kwa kuwa  ukimbizi si mzuri ’’alisema Ngenda Banka.

Majira ilipata fura ya kuzungumza na Kiongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha CNDD FDD, nchini humo Niyonashima Desire juu ya kutuhumiwa kuwasambaratisha raia ambao hudai kuwakimbia kwa tabia ya fujo akana kuwa si kweli ,kwa kuwa  wao hawana Jeshi la kuwatisha na kukiri kuwa kuna wanasiasa wanaowashawishi kutokea kwa fujo zaidi.

Aidha,Nchi ya Burundi iliingia katika machafuko baada ya Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa Pili 2015 na kusababisha warundi wengi kukimbilia katika nchia za Uganga, Rwanda na Tanzania
.

0 comments: