ZUMA ALAANI CHUKI DHIDI YA WAGENI

Polisi ya Afrika Kusini wametumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kutuliza vurugu kati ya raia na wahamiaji mjini Pretoria katika maandamano ya kupinga uhamiaji, huku Rais Jacob Zuma akilaani chuki dhidi ya wageni.
Vurugu za kuwapinga wahamiaji zimeongezeka kote Afrika Kusini zikichangiwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira, ambapo wageni wanalaumiwa kwa kuwachukulia ajira raia wa nchi hiyo na kujihusisha na uhalifu.
Takribani maduka 20 yanayomilikiwa na wageni mjini Pretoria yalivamiwa na kuporwa jana, lakini polisi haijathibitisha kama mashambulizi hayo yaliwalenga raia wa kigeni.
Rais Jacob Zuma amelaani vitendo vya vurugu vilivyozuka kati ya Waafrika Kusini na raia wa kigeni, akisema raia hao wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini wanaheshimu sheria na huchangia katika kukuza uchumi wa nchi.
"Si kweli kuwa wote wanaohusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya na na magendo ya kuwasafirisha watu," alisema Zuma.

0 comments: