RAIS MPYA WA SOMALIA AAPISHWA

Rais mpya wa Somalia ameapishwa hii leo na kutowa ahadi ya kuirudisha nchi hiyo ya upembe wa Afrika katika hadhi yake.Lakini rais Mohamed Abdullahi Mohamed ameonya kwamba itachukuwa kipindi cha miongo mingine mwili kuiweka sawa nchi hiyo.Rais Mahamed ambaye anashikilia uraia wa nchi mbili Somalia na Marekani alichaguliwa mapema mwezi huu katika hatua ya kuelekea kupatikana serikali kuu madhubuti ambayo haijawahi kuweko kwa kipindi cha robo karne.Akizungumza baada ya kuapishwa rais huyo anayjulikana pia kwa jina la Farmajo amekiri kwamba serikali yake inatarajia kukabiliwa na changamoto nyinngi lakini pia amewataka wasomali kuwa wavumilivu katika kuyafikia maenedeleo ya nchi yao na hasa kwakuwa nchi hiyo inarasilimali chache.Katika kipindi cha miaka 26 Somalia imekua katika migogoro na kukabiliwa na ukame.

0 comments: