YANGA YAVUNJA REKODI YA MIAKA 30, WASHINDA 1-0 UWANJA WA MAJIMAJI

Uwanja wa Majimaji Songea taswira ya ndani kabla ya mtanange kuanza kati ya Majimaji dhidi ya Yanga uliomalizika kwa Yanga kupata ushindi wa goli 1-0.Ripota wa Globu, Songe
 
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wametoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Majimaji mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea na kufikisha alama 43 wakiwa nyuma ya alama moja ya mahasimu wao Simba.
Mtanange huo ulioanza majira ya saa 10 kamili ilichukua dakika 15 kwa Deus Kaseke kuwainua mashabiki wa Yanga baada ya kumalizia krosi ya Haruna Niyonzima iliyopanguliwa na golikipa na kumkuta miguuni na kuachia shuti kali akiwa nje ya 18.
Yanga walionekana kutawala sehemu ya kiungo na kuweza kucheza mpira zaidi ya Majimaji lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ilishindwa kuwa makini na kumalizia mipira ya mwisho iliyokuwa ikitengwa na Juma Abdul pamoja na Haruna Niyonzima.
Katika historia ya Majimaji na Yanga katikia Uwanja huo imeweza kuvunjwa leo baada ya miaka 30 kupita bila wanajangwani hao kuondoka na ushindi huku msimu uliopita wakiambulia sare.
Kali Ongala alionekana kutumia zaidi vijana katika mchezo huu dhidi ya Yanga lakini walishindwa kuonyesha umahiri wao, na ameweka wazi kuwa bado ataendelea kuwaamini vijana hao kwani ana imani watakuja kuwa wachezaji wa kutumainiwa hapo baadae.
Huu ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu kwa Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kucheza ugenini na ameweza kuondoka na alama tatu muhimu ambapo zina faida kwake huku wakiangalia mechi ya kesho baina ya Mtibwa na Simba utakaopigwa uwanja wa Jamhuri Morogoro. 
Kwenye mechi hiyo kulitokea vioja vya aina yake kwa Timu ya Yanga kushindwa kuingia vyumbani na kubadilishia nguo pembeni ya Uwanja.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo wakati timu ya Yanga wamewasili wakiwa wamekaa kwenye mabenchi na hawakuingia vyumba vya kubadilishia nguo.
Wakati wa mapumziko timu ya Yanga wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi wakiwa hawajaingia ndani ya vyumba vya Uwanja.

0 comments: