Makala
iliyopita tumeona dondoo za malezi ya watoto na vijana wenye mafanikio
(How to Raise Successful Kids) kutoka kwa Bill Murphy. Kama tulivyoweza
kusoma dondo nne za mwanzo, msingi wa maarifa haya yanaweza kutumiwa
hasa na wazazi, walezi na mtu yeyote mwenye ushawishi katika jamii ambae
anawajibu wa kucheza nafasi yake ya kizalendo kuwajenga watoto na
vijana kuwajibika kwa maendeleo yao binafsi yenye mguso kwa jamii yake
na taifa hili katika ujumla wake.
Tuendelee na dondoo zilizobakia…
5. Mwache kila mmoja atatue matatizo lake mwenyewe. (Let others solve their own problems.)
Haimaanishi
kuwaachia watoto na vijana wakumbane na mambo magumu yenye
kuwakwamisha.Isipokuwa, kuna mengi ya kuwafanya kukua kuifahamu pale
unapowapa watoto, vijana au watu unawaongoza wewe kama kiongozi,
kujifunza namna ya kutatua matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao, na
ikitokea wamekwana na kuhitaji msaada, mzazi, mlezi au kiongozi aingilie
kati baada ya wahusika kuonesha juhudi kwanza.
“Watoto
na vijana wajue tupo kwa ajili ya kuwasaidia, ila, wape fursa wao wawe
sehemu ya kichocheo cha kuona suluhusho la changamoto za maisha”
6. Simama kama rafiki unaemkuza kiakili na si “mwokozi” (Be a mentor not a savior.)
Kuna
nyakati jambo bora ambalo linaweza kusababisha kosa kubwa na kuishi na
matokeo ya kosa hilo lililofanyika. Makosa wanayofanya watoto na vijana
yana athari ndogo ukilinganisha na makosa wanayofanya ukubwani. Hivyo
basi, ni bora watoto na vijana kujifunza kutoka katika makosa madogo
hasa pale wanapokuwa umri mdogo. Zaidi ya yote, kuruhusu watoto na
vijana wawe na maisha ya yenye mfumo wa udhibiti kutokana na kile
wanachochagua kufanya ina faida pia. Hii inadhihirisha kuwa kuna nafasi
ya kujifunza kutokana na makosa ambayo wamewahi kuyafanya katika makuzi
yao hivyo kujifunza pia kwa kuonywa na kuadibiwa pele inapobidi.
7. Jifunze kukubali kushindwa inapotokea. (Learn to embrace failure when it happens)
Imekuwa
kama msemo kwa wajasiliamali, pale ambapo kushindwa (kufeli) kunakuwa
kichocheo au fursa ya kufanikiwa. Hakuna mtu anaefanikisha jambo kubwa
maishani pale anapokuwa hana changamoto ya uwoga wa kushindwa.
Luteni
Kamanda Eric anasisitiza "Katika kushindwa, watoto na vijana wanajifunza
“kupiga msuli” dhidi ya magumu na kukabili hali ya uwoga. Kwa kupiga
picha kuwa na taswira ya kufeli kunavyoweza kutokea, watoto na vijana
wanaweza kujaribu kufanya jambo hilihilo kwa namna bora zaidi ili kupata
matokeo yanayotarajiwa.”
8. Watie moyo kuthubutu. (Encourage risk-taking)
Kuthubutu
na kufeli kuko sambamba. Watu wenye uwoga wa kupoteza kile kidogo
walicho nacho, wana uwezekano mkubwa kutofanikisha jambo lolote
maishani.
Leteni Kamanda Eric anasema “kuwa mtu Yule ambae hukuwahi kuwa, tuna wajibu wa kufanya jambo ambalo hajuwahi kufanya”
9. Ingiza mamlaka yako pale inapolazimu (Assert your authority where it's sensible.)
Leteni
kamanda Eric anawataka viongozi, wazazi na walezi wenye nia ya kuongeza
uwezo wa ushupavu kwa wale wanaowaongoza, kuwasaidia watoto na vijana
kujua, “si kila kuthubutu ni kuzuri.” Kuna nyakati tunahitaji uzoefu na
mtu mwenye mamlaka kutuonesha njia nzuri ya kupita. Jambo hili, linaweza
kufanyiwa kazi sehemu yoyote ambapo watu wanakua katika mafunzo ya kazi
au taaluma ili kuwa na ufanisi kwa yale wanayofanya maishani.
10. Onesha upendo kwa watu unaowajali (Express your love for the people you care about.)
Watu shupavu wanajua kuwa wanachokifanya kina mguso kwa watu na jamii ambayo wao wanaipenda na wanaijali.
Moja ya
njia ni kuhimiza namna ya kuonesha hisia zako za upendo kwa watoto na
vijana ili wajue moja kwa moja kuwa unawajali, unawapenda na mafunzo
wanayoyapata toka kwako ni sehemu bora ya wao kukua na il wawe watu
wenye mchango chanya katika mahali pa kazi, jamii na taifa.
Kwa kweli
inahitaji kufanyia mazoezi jambo mara kwa mara ili liwe sehemu ya tabia
na hatimae kupata mwenendo unaotarajiwa. Kwa kuwajenga watoto, vijana
au watu unaowangoza kwa misingi mizuri ya mahusiano, inaweka alama ya
uhakika wa mshikamano na kuaminiana kwa misingi ya maadili kutoka kizazi
kimoja na kwenda kingine.
Nihitimishe
makala ya leo kunukuu mafunzo kutoka kwa mfalme Suleiman. Mfalme huyu
kaandika methali nyingi sana katika vitabu vitakatifu na kuna misingi na
kanuni kaziweka ambazo zaweza kuwa nguzo ya familia, jamii na taifa
katika ujumla wake. Mfalme Suleiman amesema “Mfundishe mtoto katika njia
anayotakiwa kwenda, maana hataiacha hata atakapokuwa mzee au mtu mzima.
Dhana ya
Mfalme Suleiman inashabihiana kabisa na walimu wengi au makocha wa
maendeleo ya watu. Mmoja ya mwalimu wa maendeleo ya watu ni Dk. A. R.
Bernard ambae aliwahi kutoa tafsiri ya mafunzo. Dk. Bernard anakazia
sana mafunzo kama njia ya kuleta mabadiliko ya kitabia kwa watu na jamii
kwa ujumla. Kwa alichokisema Luteni Kamanda Eric na Dk. Bernard
tukichanganya vyote tutapata kizazi kipya chenye “akili” za ushupavu
wenye lengo la kuchangia maendeleo ya nchi hii kwa kutatua matatizo na
kubabili changamoto zilizopo na zitakazokuja.
Dk.
Bernard ametafsiri mafunzo (traning) kamakumkuza mtu kupitia maelekezo
(instructions), nidhamu (discipline) and na mazoezi ya kile
anachoelekezwa (practice).
Tanzania,
tuna nafasi ya kuzijenga familia zetu hususani watoto, vijana na wale
tunaowaongoza makazini kwa kuwafunda (mentor) katika misingi sahihi ya
kizalendo na ushupavu. Tunahitaji Tanzania ya leon na hatimae kesho iwe
na watu wenye mtazamo wa kuleta majibu kwa matatizo na changamoto. Mambo
haya hayatotokea pasipo sisi kwa pamoja kucheza nafasi zetu kwa
kuyasababisha yatokee.
Mungu Ibariki Tanzania. Kwa pamoja tunaweza kujenga vijana shupavu watakao kuwa chachu ya kulijenga Taifa letu.
Fredrick Matuja
0 comments: