MWANAMIEEREKA WA WWE JIMMY ‘SUPERFLY’ SNUKA AFARIKI DUNIA

Jimmy Snuka
Jimmy Snuka
Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka alimaarufu kama 'Superfly' amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.
Mzaliwa huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika
Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata 'mwanzilishi wa kitengo cha high flying' katika ukumbi wamiereka.
Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'Nakupenda babangu' na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.
Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.
Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.
Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.
Alikana madai hayo ya mauaji.
Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii

0 comments: