JWTZ AFA KWA KUGONGWA NA GARI MKANI KIGOMA

NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

ASKARI  Mmoja  wa  Jeshi  la kujenga Taifa( JWTZ) kambi ya Bulombola Said Hashimu (30) amekufa papo hapo baada ya kugongwa na  gari aina ya Nissan Extril yenye namba T 888 BSB iliyokuwa ikiendeshwa na David Mashauri.

Akifafanua tukio hilo Mkoani  kigoma ujiji jana Kamanda wa Polisi Mkoa huo wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema Januari 2, mwaka huu saa 4.00 usiku katika barabara ya Kigoma kwenda Kasulu ndani ya manispaa ya kigoma ujiji mkoani humo, askari huyo akiendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 271 BFV aina ya Kinglion akiwa katika barabara hiyo ndipo alikutwa na umauti huo.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kutokuwa makini na watu wengine wanaotumia njia hizo,ilihali wanajua wajibu wao pindi wanapotumia njia hizo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,ili iwe fundisho kwa wengine wanavunja sheria za usalama barabarani.

DCP Mtui alitoa mwito kwa madereva wa vyombo vya moto kufuata kanuni,taratibu na sheria za usalama barabarani,ili kuepusha vifo na majeruhi vitokanavyo na ukiukwaji wa sheria hizo,ambazo zikitumika vilivyo ni tija ya kuepuka vifo hivyo na ulemavu wa kudumu.
.

0 comments: